Katika hali ya kuwapongeza na kuwapa motisha ya kufanya vizuri zaidi katika kuinua kiwango cha Elimu Jimbo la Dodoma Mjini, Mbunge Mhe. Anthony Mavunde ametimiza ahadi yake kwa walimu wa Shule ya Msingi Mlimwa B aliyoitoa kugharamia safari ya kwenda kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro iwapo watasaidia wanafunzi kufanya vyema katika mitihani yao. Baada ya walimu kutimiza wajibu wao kikamilifu kwa ufaulu mzuri na kuifanya Shule hiyo kuongoza katika matokeo ya Darasa VII katika Shule za Serikali Jijini Dodoma. Mhe. Mavunde ametimiza ahadi yake kwa kugharamia safari ya walimu zaidi ya 30 pamoja na Mratibu Elimu Kata ya Kiwanja cha Ndege, Diwani wa Kata Mhe. Amos Mbalanga na Katibu mwenezi wa kata ambapo Mhe. Mavunde ametgharamia huduma za usafiri, chakula na malazi kwa walimu hawa kama chachu ya wao kuzidi kufanya vyema katika malezi na taaluma shuleni hapo.
Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mlimwa B, Asha Issa Maulid amemshukuru sana Mh. Mbunge kwa kutimiza ahadi yake ya safari kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro. "Tunamshukuru sana Mbunge wetu leo ametuleta hapa Ngorongoro, hii kwetu kama walimu ni shule, inatuondolea nadharia kwa sababu wengi wetu hatukuwahi kufika hapa na sasa tunakwenda kufundisha wanafunzi wetu kwa ujasiri na mifano mingi zaidi" amesema Mwalimu Asha Maulidi.
Tunamshukuru sana Mbunge na Mungu azidi kumpa afya njema katika majukumu mengi aliyonayo, alimalizia kwa kumtakia kila la heri Mbunge wa Jimbo la Dodoma.
Mheshimiwa Anthony Mavunde ni mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu Wenye Ulemavu.
Baadhi ya walimu wa Shule ya Msingi Mlimwa B wakiwa na mwongozaji wa watalii (katikati mstari wa mbele) walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.