• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mifumo ya fedha kudhibitiwa kwa fani ya Uhasibu na TEHAMA

Imewekwa tarehe: December 16th, 2022

Na. Peter Haule, WFM, ARUSHA

SERIKALI imetoa rai kwa vyuo vyote nchini vinavyo fundisha fani za uhasibu, fedha, uchumi na biashara kuhusisha Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuwa na wataalamu watakao simamia vyema mifumo ya fedha na kuondoa vihatarishi vilivyopo.

Rai hiyo imetolewa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Athumani Mbuttuka wakati wa mahafali ya 24 ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), jijini Arusha.

Mbutuka alisema kuwa mapato mengi yanakusanywa kupitia mifumo hivyo wahasibu wenye utaalamu wa Tehama wanaweza kuhakikisha kuwa mifumo hiyo ya kifedha inakuwa salama.

“Wahasibu wengi wanaweza kufanya uchambuzi mzuri wa data lakini tunauhitaji wataalamu wa uhasibu na Tehama ili kufanya kazi kwa ufanisi na kuhakikisha kunakuwa na usalama zaidi katika mifumo ya mapato hususani kwa kudhibiti wanaofuta taarifa za mapato kutoka kwenye chanzo”, alisema Mbuttuka.

Alisema kuwa vyuo vinavyotoa fani za Tehama vihakikishe masuala ya ukaguzi na fedha unakuwa sehemu ya fani hiyo ili kuondoa vihatarishi katika maeneo hayo jambo linaloweza kuongeza ajira nyingi kwa kuwa eneo la ukaguzi kuna uhaba mkubwa.

Mbuttuka alisema kuwa wakati Kenya inawataalamu wa ukaguzi wa mifumo ya taarifa waliothibitishwa 1456 Tanzania walikuwa 152, hadi Novemba, 2021 hali ambayo inaashiria kuwa Chuo cha Uhasibu Arusha na Vyuo vingine vya aina hiyo vina fursa ya kutoa wahitimu wengi zaidi wa fani hiyo na kukuza ajira nchini.

Aidha Mbuttuka amekitaka Chuo cha Uhasibu Arusha kuhakikisha wataalamu wanaoandaliwa wanakuwa mstari wa mbele katika kutoa majawabu kwa changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii, ili kuchangia katika kujenga uchumi wa nchi na wa mtu mmoja mmoja.

Alisema Serikali imeandaa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025. Miongoni mwa Malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ni pamoja na Kujenga Uchumi imara na wenye uwezo shindani na kuwaletea wananchi maisha bora.

Alisema imani ya Serikali kwa Taasisi za Elimu ya Juu ni kuona mnaisaidia katika kutimiza malengo hayo ili kuboresha viashira muhimu vya kuendeleza sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii

Pia amekipongeza chuo hicho kwa usimamizi mzuri wa fedha za umma hususani katika ujenzi wa majengo mbalimbali ikiwemo madarasa, maabara za kompyuta, hosteli na majengo ya utawala ambayo yanajengwa kwa kutumia mapato ya ndani kupitia ‘force account’.

Alisema utekelezaji wa miradi hiyo umezingatia viwango vya ubora na thamani ya fedha, jambo ambalo ni la mfano na linapaswa kuigwa na Vyuo vingine, hivyo Wizara ya Fedha na Mipango imewaunga mkono kwa kuwaongezea fedha za miradi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Mwamini Tulli, ametoa rai kwa wahitimu kuhakikisha wanachangia katika uchumi wa nchi kwa kuwa Taifa linawahitaji.

Alisema kuwa Chuo kimewapa elimu ya nadharia na vitendo hivyo wasitegemee ajira za Serikali pekee kwa kuwa mafunzo waliyoyapata chuoni hapo yanawawezesha kufanya mambo mbalimbali, jambo la kuzingatia ni kujiamini kwa kuwa uwezo wanao.

Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Cairo Mwaitete, amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassani, kwa kukipatia chuo hicho Fedha za Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kiasi cha shilingi bilioni 44. Kwa ajili ya kuboresha miundombinu na elimu ili iendane na ulimwengu wa kisasa

Alisema fedha hizo zitatumiwa na Kampasi Kuu ya Arusha, Manyara na nyingine zitatumika katika Kampasi mpya inayojengwa Songea Mkoani Ruvuma.

Katika mahafali ya 24 ya Chuo cha Uhasibu Arusha jumla ya wahitimu 3529 wamehitimu mafunzo yao katika ngazi mbalimbali ikiwemo Astashahada na Shahada za Uzamili, ambapo kati yao wanaume ni 2041 na wanawake ni 1488.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.