MRATIBU wa Mpango wa Shule Salama kupitia Mradi wa SEQUIP kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Hilda Mgomapayo ametoa rai kwa walimu wa shule za sekondari waliopatiwa mafunzo ya Programu ya Shule Salama kuhakikisha wanakwenda kuwapa mafunzo walimu wote na wanafunzi katika shule wanazotoka ili kujenga uelewa mmoja wa dhana nzima ya Mpango wa Shule Salama.
Amesema kila mwalimu kwa kushirikiana na mwanafunzi anapaswa kuwa balozi wa kuboresha mazingira ya elimu kwa kuhakikisha vitendo vyote vya ukatili na unyanyasaji vinadhibitiwa na ili kuwe na mazingira salama ndani na nje ya shule.
Akizungumza na washiriki wa mafunzo ya utekelezaji wa Mpango wa Shule Salama mkoani Mbeya wakati wa kuahirisha mafunzo hayo, Hilda amesisistiza kuwa walimu hao ni nguzo muhimu katika kuhakikisha wanafunzi wanalindwa dhidi ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji na kufanya mazingira yanayowazunguka wanafunzi kubaki salama.
Sambamba na hayo, amewaelekeza walimu hao kuzingatia utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Mpango wa Shule Salama na utunzaji wa kumbukumbu za kila kinachotekelezwa katika jalada la Mpango wa Shule Salama na kwamba Ofisi ya Rais-TAMISEMI itafanya ufuatiliaji kuona hali ya utekelezaji wa mpango huo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.