• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mkataba ujenzi Uwanja wa Mpira wa Miguu wasainiwa Dodoma

Imewekwa tarehe: February 12th, 2025

Na. Aisha Ibrahim, DODOMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Greyson Msigwa, amesema mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu Dodoma, utakaoweza kubeba watu 32,000 ambao utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 352 fedha za kitanzania, unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24, chini ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aliyasema hayo katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu Dodoma, uliohusisha wizara hiyo na Kampuni ya Lemonta SPA, iliofanyika kiwanja cha Changamani, Kata ya Nzuguni, jijini Dodoma.

Akizungumza kuhusu lengo la ujenzi wa uwanja huo, Msigwa alisema, mradi huo ni fursa kwa maendeleo ya michezo kwa wakazi wa Jiji la Dodoma kwasababu uwanja huo utatumika katika mashindano mbalimbali kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha sekta ya michezo inazidi kukua.

“Mradi huu ni fursa kwa maendeleo ya wakazi wa Dodoma lakini ni fursa kubwa kwa wanamichezo katika kukuza vipaji vyao, na sisi kama wizara tumejipanga ili uwanja huu utumike kwa mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa” alisema Msigwa.

Aidha, aliahidi kuwa atahakikisha wanasimamia mradi huo kwa umakini wa hali ya juu mpaka pale utakapo kamilika ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Mheshimiwa waziri, naomba kutoa ahadi mbele yako na mbele ya watanzania, sisi watendaji wako tutasimamia mradi huu hatua kwa hatua, kucha kwa kucha mpaka ukamilike” alisema Msigwa.

Pia, aliipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya utawala wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi na kazi nzuri inayoendelea kufanyika kwa kuhakikisha mradi huo unashughulikiwa ipasavyo mpaka kukamilika.

Nae, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, alisema kuwa Dodoma inajivunia kuwa na vivutio vingi vya utalii ikiwa ni pamoja na utalii wa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu ambapo ilikuwa ni ndoto ya muda mrefu ya wakazi wa maeneo yote ya Jiji la Dodoma kuwa na uwanja mzuri wenye viwango vya hali ya juu.

“Moja ya kipaumbele ni Dodoma kuwa mkoa wa utalii na utalii huo ni pamoja na michezo ya mpira wa miguu na tunaishi kwa imani kuwa uwanja huo utakamilika hivyo tujipange kuwa utalii wa michezo utakuwa ni tija kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma” alisema Senyamule.

Sambamba na hayo, aliongeza kuwa matarajio ya kila mkazi wa Jiji la Dodoma, ni kuona mechi za AFCON zakichezwa katika uwanja huo ikiwa ni njia mojawapo ya kukuza sekta ya michezo kitaifa na kimataifa.

“Tumekuwa tukisema kwa wananchi kuwa Dodoma, AFCON itachezwa iwe kwa mechi au kwa mazoezi lakini tunatamani matone ya AFCON yatudondokee hapa Dodoma na ndio maana wananchi kila siku wakawa wanasema hivi kweli!! uwanja upo? Yaani wanaanza kuona kama AFCON haitowahusu” alisema Senyamule.

Alimaliza kwa kusema kuwa wakazi wa Dodoma wapo tayari kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuhakikisha ujenzi wa mradi huo unatimia kwa wakati maalum uliopangwa.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.