• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mkurugenzi amshukuru Dk. Samia kwa Bilioni 1.6 za ujenzi miundombinu ya elimu

Imewekwa tarehe: May 30th, 2023

Na. Dennis Gondwe, MNADANI

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha shilingi 1,654,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ya awali na msingi jambo litakalowawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora na salama.

Shukrani hizo zilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Francis Kilawe alipokuwa akitoa salamu za halmashauri yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma aliyefanya ziara ya kikazi kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya sekta ya elimu inayotekelezwa jijini Dodoma.

Kilawe alisema “sisi Halmashauri ya Jiji la Dodoma tunamshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyoitizana kwa namna ya pekee Halmashauri ya Jiji na kutupatia miradi hii yenye thamani kubwa ya shilingi 1,654,000,000. Sisi tutazidi kuisimamia kwa ukamilifu ili malengo yaliyokusudiwa yaweze kufikiwa”.

Alisema kuwa Halmashauri ilipokea shilingi 1,654,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa shule nne mpya za msingi na vyumba vya madarasa. “Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, katika ujenzi wa shule mpya za msingi nne, leo umetembelea shule mbili ambazo ni Swaswa na Mbwanga. Shule ambazo haukutembelea ni Msalato na Mayeto.

Shule kila shule ina bajeti ya shilingi 318,800,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba tisa vya madarasa, matundu ya vyoo na kuweka madawati” alisema Kilawe.

Akiongelea ujenzi wa madarasa kupitia mradi wa BOOST alisema kuwa kuna ujenzi wa madarasa manne na matundu matatu ya vyoo katika shule ya Msingi Nzuguni B kwa gharama ya shilingi 97,100,000. “Shule ya Msingi Chang’ombe, kuna ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu matatu ya vyoo kwa shilingi 120,100,000. Shule ya Msingi Michese, kuna ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na matundu manne ya vyoo kwa shilingi 98,800,000. Mwisho ni Shule ya Msingi Kisasa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya awali na matundu sita ya vyoo kwa shilingi 68,600,000” alisema Kilawe.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Godwin Gondwe alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inaleta miradi mingi ya maendeleo katika Wilaya ya Dodoma. Halmashauri ya Jiji imepokea shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya miradi ya BOOST. Hapa Mbwanga shilingi 318,800,000 zimeletwa kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya. “Jambo kubwa miradi hii imetusaidia sana kutoa ajira katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Mama lishe wanapika chakula na kuuza kwa mafundi. Mafundi na mafunzi wasaidizi wanapata ajira za ujenzi hapa. Wauza mbao na saruji wanapata biashara kupitia miradi hii. Wauza nondo wanapata biashara na ajira kwenye miradi hii. Miradi hii inakuza mzunguko wa fedha katika Jiji la Dodoma” alisema Gondwe.

Kaimu Mkuu wa Wilaya huyo ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi alifurahishwa na ushiriki wa wananchi wa Mbwanga baada ya serikali kutoa shilingi 318,800,000 za ujenzi wa shule mpya. “Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, naomba niwapongeze wananchi wa Mtaa wa Mbwanga sababu wamemuunga mkono Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kusikia mradi huu. Wananchi wenyewe walisafisha eneo na wakapanda miti kuzunguka eneo hili kwa lengo la kulinda mipaka” alisema Gondwe.

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akiambatana na kamati yake ya Usalama alifanya ziara ya kutemebelea na kukagua miradi ya elimu katika Jiji la Dodoma akianzia Shule ya Sekondari Bunge, Shule ya Msingi Kisasa, Shule ya Msingi mpya Swaswa inayojengwa na Shule ya Msingi mpya Mbwanga inayojengwa na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo na kufanya mkutano wa hadhara kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata ya Mnadani.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.