• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mkurugenzi Mafuru atatua mgogoro uliodumu miaka 30 Dodoma

Imewekwa tarehe: May 20th, 2021

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 katika Mtaa wa Ndachi na kuwawezesha wananchi kupata hati za kumiliki maeneo yao kwa mujibu wa sheria.

Mkurugenzi Mafuru ametatua mgogoro huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye uwanja wa michezo katika Mtaa wa Ndachi uliopo Kata ya Mnadani jijini hapa. Mafuru amefafanua kuwa wananchi hao wamekosa maendeleo kwa muda mrefu kutokana na kuwa na migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu.

Aidha, Mafuru amesema kuwa wananchi wakitaka migogoro hiyo ya ardhi iishe, inaisha na pia wasipotaka migogoro iishe pia haiwezi kuisha. “Hivyo, ni vema kuchukua uamuzi wa kumaliza migogoro hiyo kwa wakati unaotakiwa ili kuweza kuleta maendeleo zaidi katika mtaa huo.

Sehemu nyingine tumeweza kumaliza migogoro kwa kutoa majina ya watu 100 halafu wanakuja ofisini tunatatua matatizo yao, hao wakimaliza wanafata wengine 100 kisha tena wanafuata 100 mpaka wanaisha na migogoro pia inaisha. Hapa pia tutafanya hivyo hivyo. Ili kumaliza tatizo ni vyema kulifuata tatizo na sio kulikimbia. Maeneo mengi tumeweza kumaliza migogoro hii ikiwemo Nzuguni, Mtumba, Michese pamoja na Nala. Wananchi wamepata haki zao, lakini Ndachi wamechelewa kutokana na migogoro iliyopo inatakiwa kuisha kwanza” amesema Mkurugenzi Mafuru.

Mkurugenzi huyo amekumbusha kuwa wakati wa upimaji walikubaliana watagawana asilimia 30 kwa Jiji na asilimia 70 kwa wananchi. Asilimia 30 ya Jiji itatumika kuwafidia wananchi ambao viwanja vyao vitakuwa vimeingia katika miundombinu kama barabara, shule na vituo vya afya.

Imeelezwa kuwa orodha ya majina ya wananchi pamoja na ramani za viwanja hivyo zimekamilika. “Tutahamishia ofisi hapa. Wataalam wetu watakuwepo hapa ili kutatua kero zote za wananchi hatua kwa hatua mpaka pale watakapozimaliza. Sisi tumekuja kulinda ardhi ya wananchi kutoka kwenye ardhi ya maneno maneno na kuwa mali halali ambayo inaitwa hati. Hii ni ardhi salama kwa manufaa ya wananchi na vizazi vyao vijavyo” alisema Mkurugenzi Mafuru.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango miji na Mazingira ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mhe. Jaffari Mwanyemba alisema kuwa wanaelekea ukingoni mwa zoezi hilo. “Ramani pamoja na majina tayari tumeshatoa. Kazi imeandaliwa na wataalamu ambao ni binadamu hivyo, kama kuna kasoro ni vizuri zikatajwa ili kutatuliwa mapema. Kama unaeneo haki haitapotea, tutahakikisha kila mtu anapata haki yake na migogoro kuisha kabisa. Niwasihi tu kufuata vile ambavyo mtakuwa mkiambiwa wakati wa kukamilisha zoezi hilo’’ alisema Mhe. Mwanyemba.

Nae mkazi wa mtaa huo, Sharifa David alipongeza juhudi za halmashauri katika kutatua mgogoro huo uliodumu muda mrefu. Alisema kuwa wanaweza kuendeleza maeneo yao na kujiletea maendeleo.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.