MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi amemaliza hofu ya kuhamishwa iliyokuwa imetanda kwa wafanyabiasha takribani 2,500 wa Soko la Sabasaba Mjini Dodoma baada ya kuwahakikishia kuwa wataendelea kufanya shughuli zao katika Soko hilo linalomilikiwa na Manispaa ya Dodoma na kwamba hakuna wa kuwahamisha.
Aliyasema hayo jana alipofanya ziara Sokoni hapo na kufanya mkutano na Wafanyabiashara hao ambao walimueleza Mkurungenzi huyo kuwa wamekuwa wakipata taarifa zisizo rasmi kuwa upo mpango wa wao kuhamishwa katika soko hilo hali inayowakosesha usingizi na kutojua hatma yao.
“Hakuna kuhama hapa ng’oo…Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ndiyo mmiliki wa Soko hili ambalo asili yake hapo awali lilikuwa eneo la Maonesho ya Sabasaba ambapo wadau mbalimbali walikuwa na vibanda vyao vya maonesho” alifafanua Kunambi huku akishangiliwa na wafayabiashara hao.
Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Kunambi alifuatana na Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede.
Wafanyabiashara hao waliishukuru Manispaa ya Dodoma baada ya viongozi hao kufika na kuzungumza nao katika wakati muafaka baada ya kufanya biashara zao kwa wasiwasi mkubwa kwa siku kadhaa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.