• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mkutano Mkuu wa 39 wa ALAT wafanyika Dodoma

Imewekwa tarehe: March 20th, 2025

Na. Aisha Ibrahim, DODOMA

Mkutano mkuu wa 39 wa Mwaka wa Mamlaka ya Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma, uliofunguliwa na mgeni rasmi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kujadili na kufanya tathmini ya mipango ya ALAT na mambo mbalimbali yanayoendelea katika serikali za mitaa.

Akitoa taarifa wakati wa mkutano huo, Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Murshid Ngeze, alisema kuwa katika mkutano wa mwaka huo wamejitahidi kualika viongozi mbalimbali wakiwemo wenyeviti wa mitaa ili kupata maarifa mbalimbali yanayohusiana na uendeshaji wa serikali za mitaa. Hivyo, kwenda kuwa viongozi bora katika mitaa yao. “Mkutano huu tunafanya kila mwaka, lakini mwaka huu tumeenda mbali zaidi kwa kuwaalika wenyeviti wa serikali za mitaa ili watakapofika hapa waweze kupata ujumbe wa moja kwa moja na kujifunza namna ya uendeshaji na utekelezaji wa shughuli zote zinazohusiana na serikali za mitaa” alisema Ngeze. 

Katika hatua nyingine, aliishukuru Benki ya NMB kwa kuwa mdau mkubwa wa ALAT na kujitoa katika kuhakikisha shughuli za serikali za mitaa zinazidi kusonga mbele na kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutekeleza miradi mbalimbali nchini. “Tunaishukuru sana Benki ya NMB kwa kuwa mdau wetu mkubwa na kwa mwaka huu ametuunga sana mkono na ifikapo tarehe 13 Machi, 2025 wajumbe wote wa mkutano huu tutakuwa tunasafiri na SGR kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kwa ufadhiri wa NMB” alishukuru.

Aidha, aliongeza kuwa ALAT imeimalika na kuwa bora kuliko miaka iliyopita kwasababu taarifa za ukaguzi zinawasilishwa mbele ya hadhara na kutolewa ufafanuzi unaojitosheleza. “Mheshimiwa Rais, kwa sasa ALAT imeimarika, mikutano iliyopita taarifa za ukaguzi zilikuwa haziwasilishwi, lakini hivi sasa taarifa hizi zinakuwa wazi na kuwasilishwa vizuri sana” aliongeza Ngeze.

Sambamba na hayo, alifafanua kuwa wamejitahidi kufuata maelekezo ya Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha ushirikiano mzuri kati ya viongozi wa ALAT na taasisi mbalimbali duniani kote. “Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwanza ulisema tuimarishe ushirikiano wa ALAT na taasisi nyingine ikiwemo; Umoja wa Serikali za Mitaa Afrika Mashariki na duniani kote. Hivyo, nikuthibitishie kwamba kauli yako tumeitekeleza kama unavyoona hapa wapo viongozi wa ALAT kutoka Zanzibar na Afrika Mashariki” alifafanua.

Pia alieleza kuwa wamejitahidi kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa. “Hapo nyuma tulikusanya kiasi cha shilingi bilioni 848 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ikiwa ni sawa na asilimia 60 ndani ya halmashauri zetu nchini, na hii yote ni kutekeleza maelekezo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan” alieleza Ngeze.

Alimaliza kwa kusema kuwa “tunafanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya ALAT, na hivi sasa tumeenda mbali zaidi kupitia mkutano huu tunakwenda kuhuisha sheria ya uanzishaji wa ALAT na iendelee kuimarika chini ya ushirikiano mkubwa kuhakikisha maendeleo ya wananchi yanatekelezeka” alisema Ngeze.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.