• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

MOI na KCMC kupasua Ubongo, Mgongo

Imewekwa tarehe: February 8th, 2021

TAASISI ya Mifupa MOI kwa kushirikiana na Hospitali ya rufaa ya kanda ya kaskazini (KCMC) leo tarehe 05/02/2020 zimeanzisha ushirikiano wa kutoa huduma za kibingwa za upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu kwa wakazi wa kanda ya kaskazini ili kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu kuafuata huduma hizo Dar es Salaam au kwenda nje ya nchi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya rufaa ya Kanda KCMC Dkt Sarah Urasa amesema ushirikiano baina ya MOI na KCMC utaleta tija kubwa sio kwa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro pekee bali kwa mikoa yote ya kanda ya kaskazini na nchi jirani ya Kenya ambao wamekuwa wakifika KCMC hapo kupata huduma.

“Kwanza niwashukuru ndugu zetu kutoka MOI ambao wamefika hapa ili tushirikiane kuanzisha huduma hizi za kibingwa za upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu, tumekuwa tukitoa huduma hizi na sio kwa kiwango kikubwa hivyo kwa kushirikiana na MOI tutakuwa tunatoa huduma hizi kwa kiwango kikubwa” Alisema Dkt.
Sarah

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amasema kuanzishwa kwa huduma za kibingwa za upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu katika hospitali ya KCMC ni azma ya Serikali ya awamu ya Tano ya kusogeza huduma za kibingwa kwa wananchi na kuwapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma Dar es Salaam.

“Tumekuja hapa kwa ajili ya kuanzisha ushirikiano na wenzetu hawa wa KCMC katika eneo la upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu ili wagonjwa wenye magonjwa hayo wapate huduma hizo hapa pasipo ulazima kuja MOI, wataalamu wetu wamekuja kufanya tathmini ili tuwashauri namna bora ya kutoa huduma na pia kuwajengea uwezo wataalam wa hapa” Alisema Dkt. Boniface

Ushirikiano baina ya MOI na KCMC unatekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya awamu ya Tano ya kusogeza huduma za kibingwa kwa wananchi ili kuwapunguzia usumbufu wa kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo Dar es Salaam au nje ya nchi.

Tangu uhusiano huu wa tiba kati ya KCMC na MOI uanze tayari wagon jwa watatu wamepata huduma hii ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu ambapo wangekwenda nje ya nchi serikali ya Tanzania ingelipa jumla ya milioni 135 wakati hapa KCMC matibabu yao yamegharimu jumla ya kiasi cha shilingi milioni 13 tu.

Kwa msaada wa Fullshangwe Blog



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.