• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Moto waua watu 68 Morogoro; tahadhari yatolewa

Imewekwa tarehe: August 11th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kebwe Stephen Kebwe amesema, hadi sasa idadi ya watu waliokufa kutokana na ajali ya kupinduka na kulipuka kwa lori la mafuta imefikia 68. Amemweleza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Morogoro kuwa, watu 62 walikufa kwenye eneo la ajali na wengine sita wameaga dunia hospitalini.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekwenda kwenye eneo ilipotokea ajali hiyo na kushuhudia mabaki ya gari lililolipuka jana saa mbili asubuhi.

Lori hilo aina ya Scania lilipinduka sehemu ya Mzambarauni eneo la Msamvu, Manispaa ya Morogoro katika Barabara Kuu ya Dar es Salaam – Morogoro jana. Ajali hiyo ilitokea saa 2:20 asubuhi ambayo mashuhuda walieleza ilisababishwa na mwendesha bodaboda aliyekuwa na abiria wake mwanamke na mtoto kukatisha barabara hali iliyomfanya dereva wa lori hilo kuwakwepa, lakini likapinduka kiubavu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Wilboad Mutafungwa amethibitisha kuwa lori lililobeba mafuta aina ya petroli likitoka Dar es Salaam kabla ya kufika Msamvu Stendi lilipinduka upande wa kushoto wa barabara. Baada ya kupinduka katika eneo hilo lenye makazi wa watu na karibu ya barabara, ghafla ukajitokeza moto mkubwa ambao ulilipuka na kuwaunguza watu wengi na takribani watu 62 walifariki dunia papo hapo kwa kuungua moto.

“Miili iliopolewa kwenye eneo la tukio na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili kuhifadhiwa na kubaini majina yao ni akina nani na ufuatiaji unaendelea ili kujua ni akina nani,” alieleza Kamanda Mutafungwa.

Alisema eneo la ajali, zaidi ya pikipiki 26 na baiskeli sita ziliteketea na moto huo na uchunguzi utafanyika ili kubaini zilifikaje hapo na kwa lengo gani, ikihisiwa walitaka kuiba mafuta yaliyokuwa yakitiririka baada ya lori kupinduka.

“Tumefanikiwa kuuzima moto huu mkali wa petroli majira ya saa nne na nusu asubuhi hii kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na wananchi pamoja na Tanesco kwa kuzima umeme maeneo haya,” alieleza Kamanda Mutafungwa.

Alisema baada ya kutokea kwa ajali hiyo, walielekeza magari ya kutoka Dar es Salaam kupita njia mbadala ikiwa na magari yanayotoka mikoa ya Iringa na Dodoma kupita njia ya zamani ya Dar es Salaam.

Kamanda Mutafungwa pia aliwaonya wananchi waliokuwa wameiba mafuta ya petroli na kuyahifadhi majumbani mwao kuyasalimisha Polisi kabla ya msako kufanyika katika maeneo hayo.

Akifafanua zaidi alisema, kwa vile gari hilo limeteketea na moto imekuwa ni vigumu kutambua namba zake, mmiliki wake ama kampuni yake, na lilikuwa linaelekea mkoa gani. Alisema uchunguzi unafanyika kubaini yote hayo. Licha ya kuungua vibaya sehemu ya mbele ya gari hilo, lakini namba za tela la mafuta zilisomeka T645 CAN.

Aidha, katika gari kulitolewa miili mitatu ambayo haijatambuliwa kama ni dereva au watu walikuwapo eneo la ajali. Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen alisema ajali hiyo imeleta maafa makubwa kwa kuwapoteza watu hao na kusababisha majeruhi wengi waliolazwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

“Nimeagiza watumishi wa hospitali na madaktari wasiende mapumziko na wale waliopo majumbani waitwe hospitali, wanapaswa kufika kazini kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa hao na kutengwa kwa wodi mbali mbali za kuwalaza,” alisema Dk Kebwe.

Mkuu wa mkoa pia alisaidia kuwahudumia majeruhi wakiwa wodini kutokana na taaluma yake ya daktari bingwa wa magonjwa ya binadamu.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood pamoja na kutoa mablanketi 100, maji na dawa vyenye kufikia thamani ya Sh milioni tano, alitumia nafasi hiyo kuwatahadharisha wananchi kuacha tabia ya kukimbilia ajali zinapotokea hasa magari ya kubeba mafuta, bali wajiokoe maisha yao kwanza.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Noel Kazimoto alisema pamoja na wadau akiwemo mbunge kutoa misaada hiyo, pia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imewasilisha ombi kwa Bohari ya Dawa (MSD) la kupatiwa dawa za dharura ikiwa na magari 10 ya kubeba majeruhi wanaohamishiwa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Rita Lyamuya alisema walipokea miili 62, kati ya hiyo 58 ni ya wanaume na wanne ni wanawake akiwamo mtoto mmoja na pia majeruhi 70 na kati ya hao, 39 walipatiwa rufaa ya kwenda kutibiwa Muhimbili.

Shuhuda Raymond Stephen alidai dereva wa lori hilo alikuwa akijaribu kukwepa mwendesha bodaboda aliyekuwa amebeba abiria mwanamke na mtoto wake, ndipo likazidi kushoto mwa barabara na kupinduka.

Stephen alisema baada ya kupinduka na wakiwa katika jitihada za kuwaokoa waliomo ndani ya gari hilo, walijitokeza watu wengi hasa wa bodaboda kwa akili ya kuiba mafuta yaliyokuwa yakitiririka kutoka juu ya tangi na chini, lakini alitokea kijana ambaye ni mtumiaji wa dawa za kulevya “teja” kuanza kuchomoa betri.

Alisema baadhi walioona watu wanazidi kuiba mafuta na “teja” huyo, wengi wao waliacha kutoa uokozi na kulikimbia eneo hilo na ndipo teja huyo alipoona anashindwa kung’oa betri hiyo, hivyo alichukua chuma na kuigonga na kung’oa kwa nguvu.

Shuhuda mwingine, Alawi Abdulrahman alidai chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa bodadoda, lakini kutokea kwa moto uliosababisha vifo na majeruhi ni mtu mmoja ambaye ni mtumiaji wa dawa za kulevya, kuichomoa betri kwa nguvu na hivyo kusababisha tangi la mafuta ya petroli kulipuka na kuleta maafa hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo alizungumza na wananchi waliofika hospitalini nakusema licha ya kuwepo kwa akiba ya damu, lakini kutokana na kiwango kikubwa cha majeruhi, walikuwa wanahitaji damu ya kutosha.

“Tumepungukiwa akiba ya damu…umejitokeza upungufu wa damu na hamjawahi kuona DC akitangaza kuomba damu. Nimekuja kwenu kuwaomba jitokezeni kutoa damu ili kunusuru majeruhi waliopo wodini,” alisema Chonjo.

Chonjo alisema kati ya majeruhi hao, 39 wanapaswa kuhamishiwa Muhimbili na madaktari wameeleza kuwa hawawezi kuwasafirisha bila kuwawekea damu, hivyo ni jukumu la kila mwananchi mwenye mapenzi mema kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha yao.

Pamoja na hayo, aliwafahamisha wananchi wa Manispaa ya Morogoro kuwa majina ya waliojeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, aliyasoma hadharani na yamebandikwa Uwanja wa Jamhuri.

Alisema baadhi ya miili 63 iliyohifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, inaweza kutambulika na ndugu zao na mingine imeungua vibaya na kwamba madaktari wameeleza kuwa ile isiyotambulika wanatumia vinasaba DNA ili kuwezesha ndugu na jamaa kuwatambua.

Baada ya kutokea janga hilo, baadhi ya viongozi waliotembela majeruhi wodini ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba pamoja na baadhi ya wabunge wa Mkoa wa Morogoro.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Liberatus Sabas na Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye walifika eneo la ajali na kuhakikisha wanashirikiana na wenyeji kufanikisha uokozi pamoja na kusaidia kwa jambo lolote linalohitaji msaada.

Hii ni ajali kubwa ya moto wa mafuta ya petroli kutokea nchini baada ya ile iliyotokea Kijiji cha Isongole wilayani Rungwe mkoani Mbeya ambayo wananchi wengi walipoteza maisha na ajali ingine ya Mbezi jijini Dar es Salaam.

Maoni yetu:

Kwa kuwa tukio hili si la kwanza kutokea na tumeona madhara makubwa kwa jamii na taifa. Tahadhari inatolewa kwa wananchi wote kuacha tabia ya kukimbilia ajali za magari ya kubeba mafuta zinapotokea, bali wajiokoe maisha yao kwanza. Wanachotakiwa kufanya ni kutoa taarifa kwenye Kituo cho chote cha Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokozi ili wafike na kusimamia uokozi. Kama itabidi wao kutoa msaada wa haraka kwa majeruhi, hawana budi kujiridhisha na usalama wa eneo husika ilipotokea ajali.

Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati lori la mafuta likiteketea kwa moto na kugharimu maisha ya Watanzania wenzetu. Ajali hii imetokea eneo la Msamvu Manispaa ya Morogoro. Ni hatari kwa mtu asiyekuwa na taaluma ya uokozi kusaidia ajali kama hii.

Chanzo: Tovuti ya HabariLeo online (habarileo.co.tz)

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.