NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini kuunda na kuenzi tunu za Taifa na kuhakikisha wanajukumu la kuja na Falsafa na Moyo wa kukuza Uzalendo Miongoni mwa Watanzania.
Wakili Mpanju amesema hayo katika siku ya pili ya kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii Novemba 09, 2022 jijini Dodoma.
Mpanju amesema Shabaha kuu ya kukuza Uzalendo nikuongeza na kuendeleza Mila na desturi kwa makusudi ya kuimarisha Taifa kwa kizazi kijacho.
"Kwa mnaokumbuka kilichokuwa IDM Mzumbe hiki ni moja ya Vyuo vilivyokuwa vikiwapika Viongozi kwa kusudio la kuwafanya kuamsha ari ya Uzalendo miongoni mwa Watanzania" amesema Wakili Mpanju.
Hata hivyo Wakili Mpanju amesema kuanzia Miaka ya 1990 hali ya Uzalendo imeendelea kulegalega nchini kutokana na watu kupoteza Uzalendo na kutokuwa na mapenzi na Nchi yao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.