WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali ipo mbioni kuanza kutekeleza mradi wa kimkakati wa uzalishaji wa gesi asilia ya kimimika (LNG) mkoani Lindi utakaogharimu dola za kimarekani bilioni 30.
Majaliwa amesema mradi huo ni mradi wa kimkakati ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepania kuutekeleza katika awamu ya sita ambao utapoanza kutekelezwa gesi hiyo itatumika kwa kipindi cha zaidi ya miaka 25.
Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Juni 5, 2021 wakati wa mkutano na wadau wa maendeleo wa wilaya ya Lindi, katika ukumbi wa hoteli ya Sea View Mjini Lindi.
“Vile viwanja mlivyovichukua anzeni kuvijenga, mradi wa gesi asilia unakuja, nina imani mradi huu ukianza baada ya kukamilisha makubaliano, tutafika hatua nzuri, jiandaeni kutumia fursa hii”, amesema.
Aidha, Waziri Mkuu amezitaka Halmashauri nchini ziongeze usimamizi kwenye sekta ambazo wananchi wanazitekeleza kila siku ikiwemo sekta ya kilimo na kuifanya kuwa moja ya agenda muhimu kwa kuwa Watanzania wengi wategemea kilimo katika kujipatia kipato.
“Halmashauri zetu nyingi watu wake ni wakulima, wafanyakazi ni asilimia tano tu na hata wafanyabiashara ni asilimia ndogo,viongozi simamieni kilimo ili kiimarishe pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla” amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.
Wadau wa maendeleo wa wilaya ya Lindi wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Sea View Mjini Lindi
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.