Na. Nancy Kivuyo, MATUMBULU
Shilingi 360,746,830 zimetumika kuboresha tanki la maji la lita 90,000 na kuweza kuwahudumia wakazi wa mitaa ya Kata ya Matumbulu huduma ya maji kwa saa 24.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea eneo la tanki hilo likiwa moja ya miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2020 hadi sasa katika Kata ya Matumbulu, Mhasibu wa Maji, Colleta Kapinga alisema kuwa mradi huo ni mkubwa na unatosheleza mahitaji ya wakazi wa mitaa mitatu ya Nyerere, Mwongozo na Kawawa. “Maji haya yanapatikana masaa 24 na kuna baadhi ya watu wanayatumia kumwagilia kilimo cha mbogamboga. Huduma hii imemtua mama ndoo kichwani. Kwahiyo, ni msaada mkubwa kwa wananchi” alisema Kapinga.
Nae Afisa Kilimo Kata ya Matumbulu, Aneth Mnana alisema kuwa upatikanaji wa maji umewashawishi wananchi kushiriki kilimo cha muda mfupi kama mbogamboga ili kujihakikishia mahitaji ya vyakula muhimu. “Tunaishukuru serikali inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huu mradi wa maji kwasababu ni mkombozi wa kilimo na unafanya kazi yetu sisi wataalam kufanyika vizuri kwasababu elimu ya vitendo inafanyika katika kuiboresha sekta ya kilimo cha kisasa” alisema Mnana.
Kwa upande mwingine mkulima wa Alizeti, Mussa Mlilima, aliishukuru serikali kwa kuwawekea mradi wa maji wenye tija na unaokidhi mahitaji. “Tunaishukuru sana serikali inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, tunamshukuru pia Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde na Diwani wa Kata yetu, Emmanuel Chibago kwa maendeleo wanayotuletea, tunawaombea kheri na afya njema ili waendelee kuchagua miradi mingine ya kugusa wananchi moja kwa moja ili kuzidisha maendeleo katika kata yetu” alishukuru Mlilima.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.