• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma atoa pongezi kwa Madiwani

Imewekwa tarehe: May 25th, 2025

Na. Nancy Kivuyo, DODOMA

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, amelipongeza Baraza la Madiwani kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi ya maendeleo katika kata zao iliyopelekea uboreshaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.

Aliyazungumza hayo katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa kupitia taarifa za utekelezaji kutoka kwenye kata 41 za Halmashauri ya Jiji la Dodoma. 

Alisema kuwa madiwani wamesimamia vizuri miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika kata zote 41. “Sisi Halmashauri ya Jiji la Dodoma tulipanga kukusanya na kutumia shilingi bilioni 143, kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 62.3 ni za mapato ya ndani. Kupitia mapato ya ndani tumetenga vilevile, kwa kuzingatia taratibu zetu asilimia 70 itumike kwenda kutekeleza miradi ya maendeleo. Kwa muktadha huo, ni busara sana tuwe na taarifa miradi hiyo imetekelezwaje” alisema Prof. Mwamfupe.

Aliongeza kuwa katika mkutano huo wa robo ya tatu walijikita katika kupitia miradi iliyotekelezwa katika kata zote na akawapongeza madiwani kwa kusimamia vizuri miradi hiyo. “Tumeangazia miradi ya aina mbili, moja ni ile miradi ilianzishwa kwa nguvu za wananchi na pili ni miradi viporo ambayo kwa kuikamilisha inatakiwa kutumika mara moja. Miradi imetekelezwa vizuri. Kwa mfano, ujenzi wa Shule ya Sekondari Matumbulu pamoja na changamoto zilizopo lakini wamefanya vizuri na miradi mingine nawapongeza sana” aliongeza Prof. Mwamfupe.


Alimalizia kwa kusema kuwa ana furaha kuona madiwani wanasimamia vilivyo utekelezwaji wa miradi ya maendeleo na kuwa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi ni wakati muafaka wa kueleza kuwa serikali imefanya yapi kwa wananchi. Bila kusahau akatoa pongezi kwa wananchi na juhudi za michango yao katika kuihimiza serikali kusogeza huduma katika maeneo yao. 

Naye Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Amos Mbalanga alisema kuwa mkutano huo umekuwa na matokeo chanja kwao kwasababu wameweza kufahamu namna miradi mbalimbali ilivyotekelezwa. “Kipekee nilipongeze baraza kwasababu katika robo ya tatu hii tumepata taarifa za namna miradi ilivyotekelezwa kwa wingi, tutaendelea kuisimamia miradi kikamilifu ili kusogeza karibu huduma kwa jamii na hilo ndio lengo letu” alisema Diwani Mbalanga.

Katika hatua nyingine, Diwani wa Viti Maalum, Flora Liacho alieleza kuwa mapitio ya miradi ya maendeleo ni jambo zuri kwasababu linawafanya madiwani kuwajibika. “Nalipongeza Baraza la Madiwani kwakuwa na desturi ya kukutana kila baada ya robo ya tatu kwasababu kama leo hii tumejadili namna miradi ya maendeleo inatekelezwa katika kata na tumeiona ile miradi kinara iliyokamilika na ipo ambayo bado ni viporo. Naamini wanaosimamia hiyo miradi viporo wataongeza kasi ikamilike kwa wakati ili wananchi wapate huduma” alipongeza Diwani Liacho.  




Matangazo

  • TANGAZO LA MABADILIKO YA TAREHE YA USAHILI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA WASIMAMIZI JIMBO LA MTUMBA October 03, 2025
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA- DODOMA MJINI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA MAKARANI WAOGOZAJI WAPIGA KURA October 03, 2025
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Rc Senyamule awasihi wawekezaji sekta binafsi kuwekeza Dodoma

    October 03, 2025
  • CCTV kamera mwarobaini wa wavunjifu wa sheria jiji la Dodoma

    October 02, 2025
  • Wadau wa afya wapongezwa kwa juhudi zakudhibiti vifo vya wajawazito

    October 01, 2025
  • UONGOZI WA KLABU YA MICHEZO OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAKUTANA NA RAS KAZUNGU

    September 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.