NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Angeline Mabula ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kutoa huduma ya matibabu ya kuvunja mawe kwenye figo na mfumo wa mkojo kwa njia ya mawimbi mshituko kwa kitaalam bila kufanya upasuaji.
Waziri Mabula alisema hayo baada ya kutembelea banda la Muhimbili kwenye maonesho ya 44 ya Sabasaba (2020) na kufurahishwa na huduma zinatolewa kwa wananchi ambapo yeye mwenyewe alipata fursa ya kupima macho na shinikizo la damu bila malipo pamoja na kupata na elimu ya afya.
Alisema kuanzishwa kwa matibabu haya ni mwendelezo wa kutekeleza juhudi za Serikali za kuboresha huduma bobezi za kibingwa nchini ili kuongeza wigo wa huduma ambazo hapo awali zilikuwa hazipatikani hapa nchini kutokana na kutowepo kwa wataalam, vifaa tiba au vyote viwili.
Huduma hii inafanywa kwa kutumia machine ambayo inatoa mawimbi sauti yanayosafiri kupitia ngozi hadi kwenye figo sehemu yenye jiwe au mawe. Mawimbi hayo hugeuka kuwa nishati yenye uwezo wa kuvunja mawe kuwa madogo mithili ya mchanga ambapo yakishasagwa yanatoka kwa njia ya haja ndogo (mkojo).
Chanzo: muhimbili_taifa (instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.