KAMPUNI ya Greenland Group ya nchini China imesaini makubaliano ya kuagiza kontena 10 za mvinyo wa Tanzania kwa ajili ya majaribio katika soko la China.
Mkataba huo umesainiwa katika Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Nje (China International Importation Expro) yanayoendelea jijini Shanghai China.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Televisheni ya Taifa ya China (CCTV) tarehe 4 Novemba, 2020 alizitambulisha bidhaa za Tanzania zinazooneshwa katika maonesho hayo ya kimataifa. Miongoni mwa bidhaa alizozitambulisha ni mvinyo, kahawa, korosho na Tanzanite.
Maonesho ya tatu ya Kimataifa ya bidhaa za nje ya China yalizinduliwa tarehe 5 na yanaendelea hadi tarehe 10 Novemba, 2020 jijini Shanghai yakihusisha nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania huku kukiwa na fursa muhimu kwa wazalishaji wa zao la zabibu kutoka Mkoa wa Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.