MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule, leo Oktoba 17, 2924, amepokea ugeni wa mwekezaji kutoka nchini Brazil katika ofisi yake iliyopo Jengo la Mkapa Jijini Dodoma.
Ugeni huo ulioongozwa na Balozi wa Tanzania nchini humo Bw. Adelardius Kilangi, umemuhusisha mwekezaji Bi Luciana Teikline ambaye ana dhamira ya kufanya uwekezaji kwenye kilimo cha Zabibu na Mvinyo Mkoa wa Dodoma utakaoleta Mapinduzi makubwa juu ya kinywaji hicho kwa kuwa Zabibu ya Dodoma imeonekana kuwa na ubora wa hali ya juu.
Miongoni mwa walioongozana na mwekezaji huyo ni wawakilishi kutoka Wizara ya Kilimo pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambapo wamepata nafasi ya kufahamu fursa kadha wa kadha zinazopatikana ndani ya Mkoa wa Dodoma mbali na uwekezaji kwenye Zabibu na Mvinyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.