MWENGE wa Uhuru mwaka 2024 utatembelea, kuzindua na kuweka jiwe la msingi jumla ya miradi saba yenye thamani ya shilingi 7,096,668,714.32 wilayani Dodoma.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri alipokuwa akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Gerald Mongela mapema leo katika uwanja wa michezo wa Shule ya Sekondari John Merlin iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Alhaj Shekimweri alisema “ninakiri kwa dhati ya moyo wangu kuupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwako Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Gerald Mongela. Aidha, ninakiri kumpokea Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa ndugu Godfrey Mnzava pamoja na wenzake watano. Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Dodoma utatembelea miradi saba yenye jumla ya shilingi 7,096,668,714.32. Vilevile, Mwenge wa Uhuru utapata nafasi ya kusalimia kongamano la vijana. Nikuhakikishie kwamba Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Dodoma tutautendea haki kwa kukimbia nao kama ratiba ilivyopangwa”.
Awali akikabidhi Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Gerald Mongela alisema “nakukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri, Mwenge huu ukiwa unawake, unameremeta na unapendeza sana. Aidha, ninakukabidhi na itifaki ya wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa sita wakiwa na afya njema wakiongozwa na Godfrey Mnzava”.
Alisema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa ndani ya Wilaya ya chemba, ulikimbizwa bila kusimama umbali wa kilometa 163 ukitembelea, kukagua na kuweka jiwe la msingi kwenye miradi sita yenye thamani ya shilingi 1,293,815,620. Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Chemba umeacha alama kubwa, aliongeza.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.