NAIBU Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde ameitaka Tume ya Kupambana na Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) na wadau mbalimbali wa masuala ya VVU na UKIMWI kuwahusisha Vijana katika kupanga mbinu za kukabiliana na ongezeko la maambukizi mapya ya VVU kwa kundi la Vijana ambapo kwa miaka ya hivi karibuni inaonesha kundi kubwa la Vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 limeathirika zaidi ambapo zaidi ya 40% ya maambukizi mapya yanawagusa Vijana katika kundi hilo.
Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akitihimisha mdahalo uliohusisha wanafunzi wa Vyuo Vya Elimu ya Juu na Elimu ya Kati juu ya mbinu mpya za kupambana na maambukizi mapya kwa Vijana, ambapo amesisitiza juu ya ushiriki wa Vijana katika kila ya mkakati wa kusaidia kutatua changamoto hii kwa Vijana ambapo kwa sasa takribani watu 200 wanapata maambukizi mapya kwa siku na 80 wakiwa ni Vijana huku 63 wakiwa ni wasichana.
"Njia hii ya majadiliano ya kuwahusisha Vijana kwenye mambo yanayowahusu wao na maslahi yao ndio njia sahihi, Vijana wapewe nafasi kutoa mapendekezo na mbinu sahihi za kutatua tatizo hili la maambukizi mapya kwa Vijana kwa kuwa wanajua zaidi mazingira yao kuliko mtu mwingine. Tuondokane na utaratibu wa kuwaamuria vijana katika mambo muhimu pasipo ushiriki wao" Alisema Mavunde
Akitoa Maelezo ya awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko amebainisha mikakati mipya ya kuwafikia Vijana kupitia matamasha ya burudani ambapo hutumia fursa hiyo kutoa Elimu kwa Vijana juu ya kujikinga na maambukizi ya VVU na pia kupata muda katika vipindi vya masomo Chuoni kutoa elimu kwa Vijana.
Picha za matukio mbalimbali:
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.