NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Deogratius Ndejembi amesema mabadiliko ya mipaka ya Maeneo ya Utawala kwa Mujibu wa Mwongozo wa Uanzishaji wa Maeneo ya Utawala katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wa Mwaka 2014 huanza na kusudio ambalo hupaswa kujadiliwa katika vikao vya Ngazi ya Halmashauri, Wilaya na Mkoa ambapo Kusudio hilo huwasilishwa Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia Katibu Tawala wa Mkoa.
Ameeleza hayo wakati alijibu Swali la Deo Sanga, Mbunge wa Jimbo la Makambako aliyetaka kujua Je, ni lini Serikali itaangalia upya mipaka ya kiutawala ikiwemo na Halmashauri ya Mji Makambako.
Ndejembi amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI bado haijapokea kusudio la kubadili mipaka kutoka Halmashauri ya Mji wa Makambako, hivyo endapo kuna uhitaji wa kubadili mipaka, inashauriwa kuanzisha kusudio na kuliwasilisha katika vikao vya Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Baraza la Madiwani, Kamati ya Ushauri ya Wilaya na hatimaye katika Kamati ya Ushauri ya Mkoa.
Aidha, Ndejembi amesema Serikali imekuwa ikizingatia suala la maendeleo ya mipaka ya maeneo ya utawala ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na kusogeza huduma karibu na wananchi.
Amesema Serikali imeweka kipaumbele katika kuendelezaji wa maeneo yaliyotengwa na kugawiwa hivi karibuni kwa kuimarisha miundombinu kama kukamilisha majengo ya halmashauri na wakuu wa wilaya pamoja na kujenga nyumba za watumishi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.