WAZIRI MKUU, Mhe. Kassim Majaliwa amekagua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Dar es Salaam hadi Kilosa, Mkoani Moroggoro na kusema kwamba ameridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa.
"Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameshamilia kukamilisha ujenzi wa miradi yote iliyoanzishwa, hivyo Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali yao, na tunawahakikishia mradi huu utakamilika kwa wakati."
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Septemba 12, 2021) wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo katika kituo cha Kwala kilichopo mkoani Pwani, ambacho kitatumika kama kituo kikuu cha kufanya matengenezo makubwa ya mabehewa na injini za treni.
"Maendeleo ya ujenzi huu yanatia matumaini na kazi inaendelea kwa ufanisi na eneo lililobaki la Pugu Dar es Salaam tunaamini litakamilika kwa wakati, nimeridhishwa na vituo vya abiria vilivyokamilika." amesema Mhe. Majaliwa.
Aidha, Waziri Mkuu amewasihi wafanyakazi wa mradi huo kufanya kazi kwa ufanisi kwani lengo la Serikali ni kuufikisha mradi huo katika mikoa ya Mwanza, Kigoma, Katavi katika bandari ya Karema.
"Njia zote za reli tunataka ziwe za kisasa, hii pia itawezesha kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, nchi yetu ni ya kimkakati kwa sababu nchi zote za jirani zinategemea reli hii."
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.