Benki ya NMB kanda ya kati wamekabidhi tracksuit jozi 150 Kwa kaimu afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Bi. Sophia Mbeyu Kwa ajiri ya timu ya Mkoa ya wanafunzi watakaoshiriki UMITASHUMITA ngazi ya Taifa yanayotarajiwa kuanza juni 5 na kutamatika juni 15 Mkoani Tabora.
Makabidhiano hayo yamefanyika na Kaimu Meneja kanda ya kati Bw. Victor Dilunga katika viwanja vya Shule ya Dodoma Sekondari na kupokelewa na Kaimu afisa Elimu Mkoa Mwl. Sophia Mbeyu.
Hatahivyo Benki hiyo wametoa vifaa hivyo ikiwa ni kurudisha Kwa jamii pamoja na kuwatangazia wanafunzi hao huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya akaunti ya Chipukizi ya watoto walio na umri wa miaka 14-17.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.