• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Ocean Road watakiwa kuanza kutumia PET-CT SCAN ndani ya mwezi mmoja

Imewekwa tarehe: December 24th, 2023

Na. WAF - Dar es Salaam

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameitaka Taasisi ya Saratani Ocean Road hadi kufikia Februari Mosi, 2024 mashine ya Pet-CT Scan iwe imeanza kutoa huduma kwa Watanzania ili rufaa za kwenda nje ya nchi zipungue.

Waziri Mwalimu ametoa tamko hilo Disemba 21, 2023 baada ya kufanya ziara ya kujionea huduma zinazotolewa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar es Salaam.

“Mmeniambia tarehe 26, Disemba mtafanya majaribio ya mashine hii sasa nataka nikija tena hapa tarehe 01-02-2024 nione mashine ya Pet-CT Sacan iwe imeanza kufanya kazi Ili Watanzania waweze kupata huduma za Pet-Ct Scan hapa nchini.” Amesema Waziri Mwalimu

Aidha, Waziri Mwalimu amemshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali Afya za Watanzania kwa kuipa fedha Sekta ya Afya kwa ajili ya matibabu ikiwemo ya Saratani Pamoja na Vifaa Tiba.

Amesema, kwa sasa wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa udhamini wa Serikali ni wagonjwa 42 wakiwemo wa Saratani wagonjwa 15 kwa muda wa miezi Mitatu kuanzia Julai hadi September Mwaka huu.

“Tunataka kupunguza Rufaa za nje ya nchi ili kusogeza huduma kwa Watanzania lakini pia kuokoa fedha za Serikali na tutaendelea kuwekeza katika kuboresha huduma za Saratani nchini.” Amesema Waziri Mwalimu

Pia, Waziri Mwalimu ameitaka Taasisi ya Saratani Ocean Road kwenda kuwajengea uwezo wataalamu waliyopo katika Hospitali za Rufaa za Kanda pamoja na Hospitali za Rufaa za Mikoa hususan huduma za mkoba kwa kuwa Taasisi hiyo ni kituo cha umahiri wa Masuala ya Saratani nchini Tanzania.

Vilevile, ameitaka Taasisi hiyo kuharakisha harakati za kufungua vituo katika Mkoa wa Mbeya na Dodoma ili watu wanaotaka kupata huduma za mionzi wazipate kwa haraka.

Waziri Ummy ameipongeza Taasisi hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa huduma za Saratani kwa Watanzania na amewahakikishia kuwa Serikali itatimiza wajibu wake ili wafanye kazi katika mazingira rafiki.

Mwisho Ametoa wito kwa Watanzania kuwa na tabia ya kupima Afya zao mara kwa mara ili kujua hali zao za kiafya mapema na kuanza kupata huduma mapema kama umekutwa na ugonjwa ikiwemo Saratani.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.