WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe Innocent Bashungwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchi nzima kusimamia kikamilifu utoaji wa huduma ya dharua katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa kuondoa urasimu unaochelewesha mgonjwa kupata huduma.
Bashungwa ametoa maelekezo hayo Mkoani Tabora katika warsha ya Sema na Mama wakati akijibu hoja na kero ya ucheleweshwaji wa huduma kwa wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma mkoani hapo.
“Utoaji wa huduma za dharura katika vituo vya kutolea huduma za afya itolewe kwa haraka, unaweza kumuhudumia mgonjwa wakati utaratibu wa kujaza taarifa lna maelezo unaendelea ili kuokoa Maisha yake, hivyo nawaelekeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusimamia utoaji wa huduma hiyo katika maeneo yao” amesema Bashungwa.
Aidha, Bashungwa amesema Serikali inatambua Machinga kuwa ni sekta rasmi ndio maana imeelekeka kuwapanga katika maeneo rafiki na kuwawekea mazingira mazuri ya kufanya biashara ambapo itakuwa rahisi kuwafikia na kuwepelekea huduma mbalimbali.
Amesema tayari Serikali imewalekeza Wakuu wa Mikoa yote kushirikiana na viongozi wa wafanyabiashara wadogo kujadili na kutafuta namna bora ya kuwapanga kulingana na mazingira ya Mkoa husika yatakayowezesha wateja wao kuwafikia.
Vile vile, amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imetoa nafasi ya upekee kwa watu wenye ulemavu katika sekta mbalimbali kama utoaji wa mikopo na ajira ambapo asilimia 3 ya nafasi za ajira zinazotolewa zimeelekezwa kwa watu wenye ulemavu.
Pia, amesema Serikali itaendelea kusimamia utoaji wa mikopo ya asilimia 10 za halmashauri kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na sasa Wakurugenzi watapimwa kwa namna wanavyotenga fedha hizo kwa mujibu wa sheria na utaratibu wa kuzigawa bila upendeleo kwa kuwanufaisha wahusika.
Warsha ya Sema na Mama iliwakutanisha viongozi wa Serikali na makundi mbalimbali ya wananchi wa mkoa wa Tabora ambao ni Machinga, Wakulima, Bodaboda na watu wenye mahitaji maalum na kupata nafasi ya kusikilizwa na kujibiwa moja kwa moja na viongozi wao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.