• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Ongezeni juhudi katika kutoa mafunzo ya Dini nchini- Majaliwa

Imewekwa tarehe: November 5th, 2022

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini nchini wakiwemo wa Jumuiya ya Kiislamu ya Istiqaama Tanzania waongeze juhudi katika kutoa mafunzo ya dini ili kupunguza au kuondoa kabisa mmomonyoko wa maadili unaoikabili jamii.

Waziri Mkuu amesema viongozi wa dini, viongozi wa umma wana wajibu mahsusi wa kuilea jamii kwa kutoa mafundisho sahihi na endelevu ya dini ili kuiwezesha kutambua na kufuata yote yaliyo mema kama ilivyo amrishwa na Mwenyezi Mungu na kuacha kabisa yote mabaya yanayomchukiza.

“Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Jumuiya ya Istiqaama na Jumuiya nyingine mbalimbali za dini ambazo zimejikita katika kutoa mafunzo ya kiroho yanayoifanya jamii kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu na hivyo kuwawezesha wananchi kuishi kwa amani.”

Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumamosi, Novemba 5, 2022) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya Istiqaama Tanzania uliofanyika ukumbi wa Mikutano wa Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Amesema hivi karibuni jamii imeshuhudia vitendo vinavyoashiria mmomonyoko wa maadili miongoni mwa Watanzania.

“Sote tumekuwa mashuhuda wa kuongezeka kwa baadhi ya vitendo viovu kama vile wazazi kuuawa na watoto wao, wanawake kuuawa na waume zao na vijana kutowaheshimu watu wazima, uvaaji wa mavazi yasiyo na stara hususan kwa wasichana na wavulana na matumizi ya dawa ya kulevya.”

“Katika suala hili la malezi, niendelee kuwasihi viongozi wa taasisi za dini kutumia vema huduma za kiroho na ibada kujenga jamii yenye tabia njema, utii pamoja na kuheshimu mamlaka zilizopo, Kwa kufanya hivyo, tutawasaidia vijana wetu kuwa raia wema, wazalendo na wenye manufaa kwa nchi yao.”

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa viongozi wa taasisi za dini nchini, kuendelea kuiunga mkono Serikali katika utoaji wa huduma za jamii hususan katika kipindi hiki ambacho Serikali imewekeza katika miundombinu bora ya afya, elimu na maji pamoja na ongezeko la Watumishi katika maeneo ya kutolea huduma nchini.

Awali, akizungumza kwa niaba ya waumini wenzake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Istiqamaa, Sheikh Seif Ally Seif, aliishukuru Serikali kwa ushirikiano inaoutoa kwa taasisi za dini na alimpongeza Rais Mheshimiwa Samia kwa kusimamia haki upendo na kujenga umoja wa kitaifa, hivyo kuifanya nchi kuendelea kuwa katika  uelekeo mzuri.

Mwenyekiti huyo alisema lengo la jumuiya ya Istiqaama ni kutoa mafundisho ya kidini na kushirikiana na Serikali katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii kama elimu ambapo wana shule 14 Tanzania Bara na Zanzibar, pia wanatoa huduma za afya pamoja na uchimbaji wa visima vya maji.







Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.