• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Osterbay Dodoma wajitokeza usafi wa mazingira

Imewekwa tarehe: May 5th, 2025

Na. Dennis Gondwe, KIWANJA CHA NDEGE

WANANCHI wa Mtaa wa Osterbay, Kata ya Kiwanja cha Ndege Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamejitokeza kufanya usafi wa mazingira katika eneo la Shule ya Msingi Mlimwa B kwa lengo la kuweka mazingira safi na kuepuka na magonjwa ya mlipuko kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji Mtaa wa Osterbay, Ashura Iberia alipokuwa akiongea na wananchi wa Mtaa wa Osterbay waliojitokeza kwa wingi kufanya usafi wa mazingira katika Shule ya Msingi Mlimwa B.

Iberia alisema “leo tumefanya usafi wa mazingira kuzunguka Shule ya Msingi Mlimwa B, wananchi wa Mtaa wa Osterbay wamejitokeza kwa wingi kufanya usafi wa mazingira. Lengo la kufanya usafi huo ni kuweka mazingira ya shule safi ili wanafunzi ambao ni watoto wetu wasome katika mazingira safi na salama. Lakini pia kuwaepusha wanafunzi na jamii inayozunguka shule hii na magonjwa ya mlipuko. Zoezi hili nimelisimamia mimi mwenyewe Afisa Mtendaji Mtaa wa Osterbay ili kutoa chachu na hamasa kwa usafi wa mazingira kwa kila mwananchi”.

Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa wa Osterbay, Hussein Ngura alisema kuwa kuanzia siku hiyo usafi ni agenda ya mtaa. “Kuanzia leo agenda yetu kuu ya Mtaa wa Ostebay ni usafi wa mazingira kama alivyosema Afisa Mtendaji wa Mtaa. Kama tutakumbuka aliwahi kufika hapa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma na kukagua usafi kwa kustukiza. Sasa hatujui ni kiongozi gani atafuata kuja kukagua, hivyo lazima tujipange kwa kuweka mazingira yetu safi. Wananchi wa Mtaa wa Osterbay mmenitendea imani kuwa nina watu kwa jinsi mlivyojitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hili la usafi wa mazingira. Pia, mimi namsifu sana Afisa Mtendaji wa Mtaa wetu kwa kazi nzuri anayofanya, hakika ni mchapa kazi hodari na anatuongoza vizuri” alisema Ngura.

Zoezi la usafi wa mazingira katika Mtaa wa Osterbay, Kata ya Kiwanja cha Ndege liliongozwa na Afisa Mtendaji wa Mtaa, na kuhudhuriwa na wenyeviti, mabalozi na mamia ya wananchi.




Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma atoa pongezi kwa Madiwani

    May 25, 2025
  • Mkopo wa 10% tija kwa maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

    May 23, 2025
  • Mkopo wa 10% tija kwa maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

    May 23, 2025
  • Wananchi Kata ya Madukani washukuru kuboreshwa huduma za Afya, Zahanati ya Chikande

    May 21, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.