• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

PM akabidhi mikopo kwa vi vikundi vya wajasiriamali Ruangwa

Imewekwa tarehe: July 8th, 2022

PM akabidhi mikopo kwa vi vikundi vya wajasiriamali Ruangwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Julai 08, 2022 amekabidhi mikopo yenye jumla ya shilingi 256,158,000 iliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa katika mwaka wa fedha 2021/2022 kwa vikundi 27 vyenye wanufaika 196.

Kati ya vikundi hivyo vya wanawake ni 14 ambavyo vimepewa mkopo wa shilingi 36,126,000. Vikundi vinane vya vijana vilipata mkopo wa shilingi 213,532,000 na vikundi vitato vya watu wenye ulemavu vilipata mkopo wa shilingi 6,500,000.

Akizungumza na wakazi wa kata ya Mandawa wilayani Ruangwa baada ya kukabidhi mikopo hiyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa matumizi mazuri ya asilimia 10 ya makusanyo yao ya ndani ambayo yanatakiwa yatolewe mkopo kwa vikundi vya vijana (asilimia nne), wanawake (asilimia nne) na watu wenye ulemavu (asilimia mbili).

Waziri Mkuu amesema uamuzi wa halmashauri hiyo kutoa mkopo huo utaviwezesha vikundi hivyo kuongeza mitaji na uwezo wa kuendeleza shughuli zao za ujasiriamali. “Vikundi vimewezeshwa kwa kuongezewa mitaji itakayoviwezesha kuzalisha kwa tija na kuweza kurejesha mikopo kwa wakati ili waweze kukopeshwa wengine.”

Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Frank Chonya amesema kati ya fedha hizo shilingi 214,658,000 zimetolewa kwa vikundi sita vya kimkakati ambapo kati yake vikundi vitatu vya vijana vinavyojishughulisha na usafirishaji wa abiria wa pikipiki vyenye wanufaika 20 vimepewa mkopo wa shilingi 57,132,000 zilizotumika kununua pikipiki 20.

“Kikundi kimoja cha vijana wa Kata ya Mandawa ambacho kina vijana 20 wanaojishughulisha na ufyatuaji wa tofali kimepewa mkopo wa shilingi 145,400,000 na kimenunua lori la tani nane litakalotumika kubebea mchanga na matofali. Pia kimenunua mashine ya kisasa ya kufyatulia matofali yenye thamani ya shilingi 25,000,000 pia kimekopeshwa shilingi 10,000,000 kama mtaji.”

Amesema ili kuwarahisishia soko, Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa itakuwa inanunua matofali kutoka kwa vijana hao kwa ajili ya ujenzi miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika wilaya hiyo. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya na elimu.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa vikundi vingine viwili vinavyojishughukisha na ufugaji kuku vyenye wanufaika 17 vilipewa mkopo wa shilingi 12,126,000 uliowawezesha kununua kuku 800 pamoja na vyakula vya kuku na dawa. “Pamoja na kutoa mikopo kwa vikundi vya kimkakati halmashauri imeendelea kutoa mikopo kwa vikundi vidogovidogo.”

Amesema mikopo yenye thamani ya shilingi 41,500,000 imetolewa kwa vikundi 20 vyenye wanufaika 133 ambapo kati yake vikundi vya vijana vinne vyenye wanufaika 22, wanawake vikundi 12 vyenye wanufaika 95 na vikundi viwili vya watu wenye ulemavu vyenye wanufaika 16. “Kupitia utoaji huu wa mikopo jumla ya ajira 452 zimepatikana katika mwaka wa fedha 2020/2021 na mwaka 2021/2022 hivyo kupunguza uzululaji, uhalifu na utegemezi kwa vijana.”

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mandawa Issa Lipei ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.