• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Prof. Shemdoe awataka wahitimu kutumia fursa za kiuchumi

Imewekwa tarehe: December 2nd, 2022

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe amewataka wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (KFDC) kutumia fursa zilizopo kujiajiri ili kuongeza kipato na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, jamii na Taifa kwa ujumla.

Hayo aliyasema kwenye sherehe za mahafali ya 50 ya KFDC zilizofanyika katika uwanja wa Shirikala Elimu Kibaha, Mkoani Pwani.

“Ndugu wahitimu, leo hii mnahitimu mafunzo yenu ya miaka miwili hapa chuoni pia wapo wale wanaohitimu mafunzo ya miezi mitatu yaliyotolewa kwa njia ya masafa ambayo yamewanufaisha wananchi wengi, nilipopita kwenye maonesho ya fani nimeshuhudia jinsi vijana mlivyoiva kiufundi katika fani mbalimbali. Nawapongeza sana kwakupata ujuzi katika fani hizo natarajia kuwa ujuzi mliopata chuoni hapa mtautumia popote mtakapo pata ajira au mtakapokuwa mmejiajiri” alisema Prof.Shemdoe.

Prof.Shemdoe aliwaeleza wahitimu kuwa ujuzi walioupata ukawasaidie kupiga hatuazaidi kimaisha na kuwataka kujiunga kwenye vikundi ili kuweza kupata fedha zamitaji kupitia mikopo ya asilimia kumi ya mapato kwenye kila Halmashauri ambazohazina riba yoyote.

“Waliopataujuzi wa ufundi uwashi muende kuomba kazi za miradi katika Halmashauri zetu kwakuwa mna ujuzi na vyeti huko kuna miradi mingi ya ujenzi” alisema Prof.Shemdoe.

Awali akitoa taarifa ya KFDC Mkuu wa Chuo hicho, Joseph Nchimbi ameeleza kuwa chuo hichokinatoa mafunzo ya fani za ujuzi wa aina mbalimbali pia alieleza jumla yawanachuo 383 wa kozi ndefu wakiwemo 235 mwaka wa kwanza na 170 mwaka wa pili.

“Chuo kimefanikiwa kuanzisha kozi fupi zaidi ya kumi ambazo zinatolewa kwa njia yakiswahili na kuwafikia idadi kubwa ya wanufaika kwa wakati mmoja,” alisema Nchimbi.

Nchimbi amefafanua mafanikio ya chuo kwa kutoa mafunzo ya nadharia na vitendo kwa wanafunzi wa muda mrefu na muda mfupi na kufanya vizuri katika mitihani yao ya VETA na wahitimu kupata ajira katika taasisi mbalimbali na kujiajiri pia.

“Fani zinazotolewa na KFDC ni ufundi bomba, ufundi wa umeme majumbani, ufundi wa magari, ufundi wa uungaji na uundaji vyuma, ufundi wa uwashi, ufundi wa useremala, ufundi wa ushonaji nguo na ubunifu wa mavazi, kilimo cha bustani na mazao mbalimbali, ufugaji, hotelia na udereva,” alisema Nchimbi.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.