• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Rais Dkt. Magufuli asisitiza kuharakishwa kwa matumizi ya kiswahili mahakamani

Imewekwa tarehe: February 2nd, 2021
  • Ampongeza Jaji Galebu kwa uandishi wa hukumu kwa Kiswahili, amteua kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani
  • Apongeza maboresho ya Mahakama ndani ya miaka 100 ya Mahakama Kuu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa rai kwa Mhimili wa Mahakama kuweka mkakati wa kutumia lugha ya Kiswahili mahakamani kwa manufaa ya wananchi huku akimpongeza na kumteua Jaji Zephrine Galeba kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa kuonyesha uzalendo wa kuandika hukumu kwa kutumia Kiswahili.

Rais Magufuli ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma jana, alisema kuwa Kiswahili ni miongoni mwa lugha kubwa duniani, ambayo inatumiwa na Watanzania wengi.

“Nitumie fursa hii, kumpongeza sana Mheshimiwa Jaji Galeba wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma kwa kutumia Kiswahili katika kutoa hukumu kwenye Kesi ya North Mara Gold Mine dhidi ya Gerald Nzumbi katika kesi ya Mapitio Na. 23 ya Mwaka 2020. Huyu ni Mzalendo wa kweli wa lugha ya Kiswahili kwenye Mahakama. Na kwa sababu ya uzalendo wake, kuanzia leo, namteua kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa,” alisema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais alisema kuwa kushindwa kuitumia Lugha hii kwenye masuala ya Kimahakama na Kisheria sio tu kunawanyima haki wananchi, bali pia kuwaongezea gharama kupitia ukalimani wa kutafsiri hukumu na mienendo ya kesi.

Aliendelea kwa kutoa rai kwa kuwasihi wadau wote wa Mahakama, ikiwemo Mahakama, Bunge, Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuandaa Mkakati wa kuwezesha lugha ya Kiswahili kwenye masuala ya Sheria na Mahakama, ikiwemo kuendelea kuzitafsiri Sheria za zamani na kutunga Sheria mpya kwa lugha ya Kiswahili.

Kwa upande mwingine, Mhe. Rais alizungumzia pia tatizo la ucheleweshaji wa mashauri kuwa bado lipo, hususan mashauri yanayohusu masuala ya biashara na mikopo ambayo yanazorotesha ukuaji wa uchumi wa nchi.

“Ipo tabia ya baadhi ya wateja wa Benki kukimbilia Mahakamani na kufungua kesi nyingi au kuweka mazuio kwa lengo la kuchelewesha urejeshaji wa mikopo wanayodaiwa na benki. Kesi za namna hiyo zipo nyingi, na nyingine zina zaidi ya miaka mitano hazijaamuliwa,” alieleza Mhe. Rais.

Alitoa mifano ya kesi zilizofunguliwa Mahakamani na wateja wakubwa wa Benki nne ambazo ni Benki ya Posta Tanzania (TPB), Benki ya Azania (Azania Bank Ltd) na Benki ya Maendeleo (TIB).

“Hali hii ya wadaiwa kukimbilia Mahakamani na kesi kuchelewa kutolewa maamuzi, imekuwa na athari nyingi za kiuchumi kwa nchi yetu. Baadhi ya athari hizo ni kupungua kwa uwezo wa benki zetu kutoa mikopo kwa wateja; na kuongezeka kwa gharama za riba kutokana na benki kulazimika kuongeza riba na kadhalika,” alieleza.

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Desemba 31, 2020 inaonyesha kuwa Azania Bank Ltd ina kesi 36 zilifunguliwa na wadaiwa wake zenye thamani ya shilingi bilioni 352.27; Benki ya Maendeleo (TIB) ina kesi 44 zenye thamani ya shilingi bilioni 167.267; Benki ya TPB ina kesi 16 zilizofunguliwa na wadaiwa wake zenye thamani ya shilingi bilioni 6.2; CRDB ina kesi 282 zenye thamani ya shilingi bilioni 113.25.

Akizungumzia Maadili ya Watumishi wa Mahakama, Mhe. Rais alimpongeza Mhe. Jaji Mkuu kwa hatua za kinidhamu zilizochukuliwa na Mahakama dhidi ya Maafisa wake wanaoichafua Taasisi huku akitoa wito kwa Kamati za maadili za Maafisa wa Mahakama za Mikoa na Wilaya kukutana.

“Hata hivyo, nimesikitika sana na taarifa kwamba, Kamati za Maadili za Maafisa wa Mahakama za Mikoa na Wilaya, ambazo kisheria zinaongozwa na Wakuu wa Mikoa na Wilaya zimekuwa hazikutani; na hivyo, kushindwa kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wenye makosa. Napenda kutumia fursa hii kuagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya wote kuhakikisha Kamati hizo za Maadili zinakutana ili kujadili masuala ya maadili ya watumishi wa Mahakama. Naagiza pia Wakuu wote wa Mikoa kuwasilisha Ripoti ya Vikao vya Kamati hizo mwezi huu,” alisisitiza Mhe. Rais.

Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameiomba Serikali na Bunge kuyapa kipaumbele mahitaji ya Mahakama yaliyooneshwa katika mpango wa miaka mitano wa maendeleo ya miundombinu ya Mahakama 2016/17-2020/2021 itakapojadili na kupitisha Mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano.

“Mhimili wa Mahakama peke yake hauwezi kutatua changamoto bila kuwezeshwa na Mihimili ya Serikali na Bunge inayosimamia rasilimali za aina zote, hapa napenda kutambua namna mihimili ya Serikali na Bunge ilivyokubali jukumu la kutatua changamoto zinazoikabili Mahakama ya Tanzania”, alisema Jaji Mkuu.

Kwa mujibu wa Prof. Juma, mfano wa Mhimili wa Mahakama kuwezeshwa na Serikali ni kukamilishwa kwa mazungumzo na Benki ya Dunia kuhusu namna ya kusaidia kuendeleza juhudi za maboresho ya utoaji huduma za Mahakama kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha za kuboresha shughuli na huduma za Mahakama.

Mwaka 2016, Benki ya Dunia iliridhia kuisaidia Mahakama ya Tanzania kupitia Serikali ya Tanzania kupata fedha za mkopo wenye masharti nafuu uliogharimu Dola za Marekani milioni 65 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 139.5 za kitanzania.

Akizungumzia namna mhimili huo ulivyowezeshwa, Jaji Mkuu alisema miongoni mwa mafanikio yaliyotokana na uwezeshwaji huo ni kukamilika kwa ujenzi wa majengo ya Mahakama Kuu kanda za Kigoma na Musoma. Aliongeza kuwa, Mahakama inatarajia kukamilisha ujenzi wa majengo ya Mahakama Kuu nyingine sita katika miji ya Mwanza, Arusha, Dodoma, Morogoro pamoja na wilaya za Temeke na Kinondoni mkoani Dar es salaam.

Alisema katika kuendelea kusogeza huduma za Mahakama karibu zaidi na wananchi, Mahakama ya Tanzania inatarajia kuanza ujenzi wa majengo ya Mahakama za wilaya 25 katika mwaka wa fedha 2020/21. Alisema ujenzi huo utawapunguzia mzigo wananchi ambao hulazimika kupata huduma kwenye Mahakama za wilaya jirani.





Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.