WAZIRIMKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza Maadhimisho yaMiaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa Mwaka 2024 yafanyike katika ngazi yamikoa na Fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya Maadhimishohayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii.
Amesema kuwakila mkoa uhakikishe Wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii ikiwemo upandajimiti, usafi wa mazingira katika maeneo ya kijamii kama vile kwenye Masoko,Hospitali, Kambi za wazee na wenye mahitaji maalum, mashindano ya michezombalimbali pamoja na makongamano na midahalo ya kujadili maendeleo endelevuambayo nchi yetu imefikia katika kipindi cha miaka 63 ya Uhuru.
Amesema hayoleo Jumatano Katika kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyikakatika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma. “Sherehe za Mwaka huu hazitakuwa naGwaride na Shughuli nyingine za Kitaifa”.
Amesema kuwaSerikali inatoa wito kwa Wananchi kushiriki katika shughuli hizo ili kujivuniasifa za kipekee ambazo zimetokana na Uhuru wetu. “Ninatoa rai kwa Wakuu wote waMikoa ya Tanzania Bara, kuzingatia na kufuata ipasavyo maelekezo Mahsusi yaliyotolewana Serikali ili kuhakikisha Maadhimisho haya yanafanyika kwa ufanisi kwa lengola kuuenzi Uhuru wetu.”
Ameongezakuwa shughuli za Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara ya Mwaka2024 zilishaanza tangu tarehe 02 na zitafanyika mpaka tarehe 09 Desemba, 2024Siku ya kilele.
“KatikaMaadhimisho haya, Taasisi zote za Serikali na Vyombo vyote vya Ulinzi naUsalama zinaelekezwa kuhakikisha Majengo yote ya Serikali Tanzania Barayanapambwa kwa vitambaa vya rangi ya Bendera ya Taifa, picha rasmi ya Baba waTaifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye ni Muasisi wa Uhuru wetupamoja na picha ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania”.
Kauli Mbiuya Maadhimisho hayo ni: Miaka 63ya Uhuru wa Tanzania Bara: “UONGOZI MADHUBUTI NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI NIMSINGI WA MAENDELEO YETU.”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.