• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Rais Dkt. Samia anataka kuona sekta ya Mifugo ikileta mapinduzi ya kiuchumi- Majaliwa

Imewekwa tarehe: December 19th, 2022

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ana mapenzi ya dhati na Sekta ya Mifugo na anatamani kuona inaleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kukuza zaidi pato la wananchi, kutoa ajira na kuchangia pato la Taifa bila kuathiri mazingira na maendeleo ya sekta nyingine.

Kutokana na dhamira hiyo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, Waziri Mkuu ameielekeza Wizara ya Mifugo na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya tathmini ya maeneo ya ufugaji yaliyopo katika maeneo yao na kiasi cha mifugo kinachoweza kufugwa na endapo mifugo itazidi uwezo wa eneo husika, wafugaji waelekezwe kuvuna mifugo yao.

Majaliwa ametoa maelekezo hayo leo (Jumatatu, Desemba 19, 2022) alipofungua mkutano wa siku mbili wa wadau wa Sekta ya Mifugo unaofanyika katika ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma wenye dhima isemayo “Mwelekeo Mpya wa Sekta ya Mifugo Nchini.

“Wafugaji wahamasishwe kuvuna mifugo yao kwa wakati ili kuwawezesha kupata bei nzuri sokoni pamoja na kupunguza changamoto za malisho hususan wakati wa ukame. Kwa ujumla kasi ya uvunaji wa mifugo nchini bado ipo chini ya asilimia 10 ikilinganishwa na viwango bora vya uvunaji wa mifugo kitaifa ambavyo ni kati ya asilimia 20 na 25.”

Waziri Mkuu amezielekeza Wizara ya Ardhi na Mamlaka za Serikali za Mitaa zihakikishe zinashirikiana na wadau wa sekta ya mifugo katika kuandaa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya vijiji na kutenga maeneo ya malisho ya pamoja, ranchi za vijiji na vitalu kwa ajili ya wafugaji binafsi.

Majaliwa amesema kuwa kwa vijiji vyenye ardhi ya kutosha, vitenge maeneo ya Ranchi za Vijiji zenye ukubwa wa kati ya hekta 200 na 500 ambazo zitatumika kwa utaratibu wa kuwapanga wafugaji kutoka ndani ya kijiji husika.

“Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambayo inamiliki Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) ihakikishe maeneo yote ya NARCO yaliyoko kwenye mikoa yetu, Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa kwanza mtambue maeneo hayo yanamilikiwa na nani na mjue yapo katika wilaya gani na yana ukubwa upi na je matumizi ni sahihi kama Serikali inaotaka.

Kwa sababu tuna watu binafsi wamechukua ardhi hiyo kazi yao ni kukodisha watu wengine, tumewaacha wafugaji wenye ng'ombe na tunawajua huyu ana ng'ombe wake 200 huyu ana ng'ombe wake 300 na tuna eneo la NARCO zuri tu badala ya kumpa hyu mwenye ng'ombe tumempa mtu ambaye hana ng'ombe tumempa mtu ambaye hana ng'ombe alafu anakuja kumpangisha mwenye ngombe. Hii Wakuu wa Mikoa tuikatae wazi.”

Pia, ameiagiza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau na wafugaji kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha mabadiliko ya mfumo wa ufugaji ikiwemo ufugaji wa kukaa katika eneo moja bila kuhamahama na wafugaji kulima malisho badala ya kutegemea malisho ya asili peke yake.

“Viongozi na watendaji wa Serikali, hakikisheni mnashirikiana kwa karibu na wadau wakiwemo wafugaji katika kuwekeza na kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya mifugo ikiwemo majosho, malambo, visima vya maji na maeneo ya malisho.”

Waziri Mkuu amesema kuwa uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora za mifugo uimarishwe ili kuongeza tija katika sekta ya mifugo sambamba na kuwahamasisha wafugaji kutumia mifugo bora iliyofanyiwa utafiti na kuonesha kuwa na tija zaidi.

Pia, Majaliwa ameelekeza wizara husika kuimarisha huduma za ugani kwenye sekta ya mifugo kwa kuweka vigezo vya kupima utendaji kazi na kuwafuatilia Wagani wote nchini ikiwa ni pamoja na kuhimiza matumizi ya TEHAMA, kuendelea kuwapatia vyombo vya usafiri na mafunzo rejea kuhusu teknolojia mpya za ufugaji wenye tija na wa kibiashara.

Aidha, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Mifugo na Uvuvi ishirikiane na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kutatua migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi. Pia wafugaji waelimishwe na kuhamasishwa kufuga kulingana na maeneo waliyonayo na kufuata sheria za nchi.

Awali, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki alisema lengo la mkutano huo ni pamoja na kuwaleta pamoja wadau wa sekta ya mifugo kujadili kwa kina na uwazi kuhusu mwelekeo mpya wa sekta ya mifugo nchini na kuwajengea uwezo wafugaji ili wafuge kwa tija na kibiashara kama wawekezaji kwenye sekta ya mifugo.

Pia, Waziri Ndaki alisema Sekta ya Mifugo inakabiliwa na changamoto mbalimbali, hivyo watatumia mkutano huo kujadili namna ya ufugaji bora pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. “Tumepanga namna ya kuwafikia wafugaji na kuwaelimisha juu ya matokeo ya athari hizo kwani sehemu kubwa ya mifugo imeathirika.”

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.