RAIS wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikaliitaendelea kuwashirikisha wanawake kwa kuhakikisha inatanua mtandao wa wanawakekatika sekta mbalimbali.
Rais Dkt. Samiaamesema hayo leo katika Kongamano la Nne la Wanawake Vijana wa Mtandao waViongozi Wanawake Barani Afrika (African Women Leaders Network – AWLN)lililofanyika Zanzibar.
Aidha, Rais Dkt. Samiaamesema lengo la kuwashirikisha wanawake ni kuweza kufikia Ajenda ya 2030 yaMaendeleo Endelevu, Ajenda ya Umoja wa Afrika ya 2063 pamoja na Dira yaMaendeleo ya Tanzania ya 2025.
Rais Dkt. Samia piaamesema maendeleo ya wanawake yamekuwa yakiathiriwa na changamoto mbalimbalikama kutokupata rasilimali, kutengwa, kutokupata haki zao na kutokupewa nafasikatika kufanya maamuzi.
Vilevile, Rais Samiaamesema takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2021 idadi ya wanawake walioajiriwailishuka ambapo wanawake milioni 45 duniani waliondoka katika ajira mwaka 2021na hivyo kuwafanya kuwa maskini zaidi.
Hata hivyo, Rais Dkt. Samiaamesema Tanzania inafanya jitihada ya kuwashirikisha wanawake katika vyombo vyakufanya maamuzi akitolea mfano kuongezeka kwa idadi ya Wabunge kutoka 21.5%mwaka 2005 hadi 37% mwaka 2022 na Mawaziri 9 katika Baraza la Mawaziri.
AWLN ni mtandao ambaounataka kuhakiksha kuwa wanawake wana sauti katika nyanja zote za maisha kwakutekeleza Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na kufikia Malengo ya AU yakufikia Afrika tunayoitaka.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.