• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Rais Samia agawa neema ya mashamba 11 kwa wananchi Kilosa

Imewekwa tarehe: June 8th, 2021

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshusha neema kwa wananchi wa Kilosa kwa uamuzi wa kufuta jumla ya mashamba 11 yenye ukubwa wa ekari 24,119 katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro na kugawiwa kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za kilimo, ufugaji na uwekezaji.

Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia ufufuaji wa mashamba 49 yenye ukubwa wa ekari 45,788.5 yaliyotaifishwa miaka ya nyuma huku na wananchi wakiwa hawana uhakika nayo ambapo Mhe. Rais ameelekeza sehemu kubwa ya mashamba hayo kutumiwa na wananchi kwa shughuli za kilimo.

Uamuzi huo wa Rais Samia Suluhu Hassan umetangazwa jana tarehe 7 Juni 2021 wilayani Kilosa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofati na viongozi, watendaji na wananchi wa kijiji cha Kimamba wilayani Kilosa wakati wa ziara yake mkoani Morogoro. 

Hata hivyo, Waziri Lukuvi alisema pamoja na kufutwa mashamba hayo haimaanishi kama yako huru kwa kila mtu kujichukulia bila utaratibu na timu maalum imeundwa kwa ajili ya kupanga matumizi ya ardhi katika mashamba hayo na kutahadharisha asitokee mtu yeyote kuzuia timu hiyo kufanya kazi yake.

“Lazima tupange matumizi ya mashamba yaliyofutwa na utaratibu utaelekezwa na viongozi wa mkoa na wilaya na isitokee mtu kuja kujigawia mashamba na kila kipande cha ardhi kitapangwa na lazima ijukikane nani anamiliki” alisema Lukuvi.

Akielezea zaidi kuhusiana na mashamba 49 yenye ukubwa wa ekari 45,788.8 yaliyofufuliwa, Waziri Lukuvi alisema ekari 30,672.2 kati ya hizo lazima zirudi kwa wananchi na ekari 15,116.3 zilizobaki zipangiwe kwa ajili ya matumizi ya uwekezaji.

Kwa mujibu wa Lukuvi, wananchi watakaopewa mashamba ni wale wasiokuwa na ardhi kabisa na asingependa ardhi itolewe kwa watu wenye nia ya kujilimbikizia maeneo na kusisitiza anachotaka ni mashamba yasaidie wale wananchi wa Kilosa kwa kujipatia kipato na kuinua maisha.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shighela alimshukuru Mhe. Rais kwa uamuzi wa kufuta na kufufua mashamba katika wilaya ya Kilosa na kueleza kuwa sasa mkoa wake unaenda kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa upangaji  matumizi ya mashamba hayo.

Alisema, hatasita kuchukua hatua kwa viongozi wa ngazi za vijiji watakaohusika kwa namna moja ama nyingine kuondoa utulivu wakati wa zoezi la kupanga matumizi ya mashamba yaliyofutwa na hatua hizo zitachukuliwa hata katika ngazi ya chama kwa watakaohusika.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kilosa ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi mbali na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi aliyoyachukua kufuta mashamba 11 na kuridhia sehemu kutolewa kwa wananchi, alisema uamuzi uliofanywa na Rais unawagusa wana Kilosa hasa wana Kimamba na kuwataka kumuumga mkono kwa juhudi anazofanya kuwatumikia wananchi.

Baadhi ya mashamba yaliyofutwa ni pamoja na Sumagro Ltd lililopo Madoto na lenye ukubwa wa ekari 7,712,  Bumagro Ltd  Kivungu ekari 5,660, M/S Sino Development (T) Ltd lililopo Kimamba ekari 6,945, Abdalah Islam lililopo eneo la Dodoma Isanga ekari 307, Mifugo Magairo la Magole lenye ukubwa wa ekari 489 na shamba la MS Masoni Company lililopo Magole ekari 466.

Mengine ni Mitibora (T) Ltd ekari 511 eneo la Magoli, Abdalah Islam ekari 307 Isanga Dodoma na Ibrahim Magairo mwenye shamba lenye ukubwa wa ekari 516 lililopo eneo la Magole.

Katika mwaka wa fedha 2020/2021 jumla ya mashamba 123 yalihakikiwa katika wilaya za Kilosa, Mvomero na Morogoro DC na kati yake mashamba 11 yenye ukubwa wa ekari 24,119 yalibatilishwa na Mhe. Rais kutokana wamiliki wake kukiuka taratibu za uendelezaji.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.