RAIS wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan jana amefanya ziara ya kushtukiza kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Tanzanite linalojengwa eneo la Selander Jijini Dar es Salaam.
Rais Samia alipata maelezo ya ujenzi wa daraja hilo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mhandisi Rogatius Mativila ambaye alisema ujenzi wa daraja hilo umefikia asilimia 98.44 na linatarajiwa kukamilika Desemba 14 mwaka huu.
Mhandisi Mativila alisema daraja hilo litakapokamilika litapunguza msongamano wa magari, ajali za barabarani, litaboresha hali ya maisha Jijini Dar es Salaam pamoja na kupendezesha jiji hilo na pia kuwa sehemu mojawapo ya kivutio cha utalii katika fukwe zilizo karibu na daraja hilo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.