RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 03 Mei, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula.
Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma ambapo Mhe. Rais Mstaafu Obasanjo ametoa salamu zake za rambirambi kwa Mhe. Rais Samia kufuatia vifo vya waliokuwa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Hayati Benjamin William Mkapa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli waliofariki dunia tarehe 23 Julai, 2020 na tarehe 17 Machi, 2021 mtawalia.
Mhe. Rais Obasanjo amempongeza Mhe. Rais Samia kwa kupokea kijiti cha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amemtakia heri katika majukumu yake.
Aidha, katika mazungumzo hayo viongozi hao wamezungumzia hali ya usalama Barani Afrika na umuhimu wa Wakuu wa Nchi kujadiliana na kutafuta suluhisho la migogoro hiyo ambayo inasababisha vifo vya watu wasio na hatia hasa wanawake na Watoto.
Pia viongozi hao wamezungumzia masuala ya maendeleo hasa katika uchumi na kusisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuongeza ushirikiano na kuondoa vikwazo vya biashara na uwekezaji.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo (kushoto) mazungumzo yaliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia).
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.