• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Rais Samia ammwagia sifa lukuki Hayati Dkt. Magufuli

Imewekwa tarehe: March 22nd, 2021

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suhulu Hassan leo tarehe 22 Machi, 2021 amewaongoza Watanzania, Wakuu wa Nchi na Serikali, wawakilishi wa mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa na viongozi mbalimbali kutoa heshima za mwisho Kitaifa kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Akizungumza katika tukio hilo, Mhe. Rais Samia amewashukuru Waheshimiwa Marais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na wawakilishi wa Wakuu wa Nchi waliokuja kuungana na Watanzania katika kutoa heshima zao za mwisho kwa Hayati Dkt. Magufuli na ameeleza kuwa ujio wao na jinsi Watanzania walivyoonesha mapenzi yao tangu msiba huu mkubwa wa Kitaifa ulipotokea vimedhihirisha kuwa Dkt. John Pombe Magufuli alikuwa kipenzi cha watu.

Mhe. Rais Samia amesema Hayati Dkt. Magufuli alikuwa mwalimu, kiongozi na mlezi wake na kwamba alihusudu utendaji wake kwa namna alivyokuwa mfuatiliaji na msimamizi wa miradi.

Amebainisha kuwa Taifa limepoteza kiongozi mahiri, shupavu, jasiri, mchapakazi, muadilifu, mnyenyekevu, mcha Mungu, mfuatiliaji, mzalendo kwa Taifa lake, mtetezi wa wanyonge, mwanamwema wa Afrika, mwanamageuzi mahiri, mwanamapinduzi wa kweli, mtu asiyekuwa na makuu na mtumishi wa wote.

Mhe. Rais Samia ameeleza kuwa wakati wa uongozi wake, Hayati Dkt. Magufuli aligusa maisha ya watu wengi na kwa muda mfupi, na kwamba kwa kipindi alicholiongoza Taifa alijikita kujenga uchumi wa ndani unaotegemea mapato ya ndani, kusimamia rasilimali za Taifa ili zifaidishe wananchi kwa kuziba mianya ya rushwa na upotevu wa mapato, kufufua na kuwekeza katika miradi ya kimkakati kama vile kufufua Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) kwa kununua ndege na ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere, ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge railway – SGR) ili kufanikisha azma ya ujenzi wa viwanda ambavyo vinahitaji miundombinu wezeshi.

Amesema katika kipindi chake cha uongozi, Tanzania ilipata Makamu wa Rais mwanamke ambaye leo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amewahakikishia Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuwa yeye na viongozi wenzake wapo tayari kuendeleza kazi nzuri iliyofanywa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na kwamba yale aliyoyakusudia yatafikiwa.

Mhe. Rais Samia amewaondoa shaka walio na wasiwasi juu ya hatma ya Tanzania baada ya Hayati Dkt. Magufuli kufariki dunia kuwa kila kitu kitakuwa sawa “Kwa wale ambao wana mashaka mwanamke huyu ataweza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nataka niwaambie aliyesimama hapa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

Amewataka Watanzania kumuenzi Hayati Dkt. Magufuli kwa kutekeleza yote mazuri aliyoyafanya katika ujenzi wa Taifa.

Ameihakikishia familia ya Hayati Dkt. Magufuli kuwa Taifa linatambua mchango mkubwa ambao ameutoa na kwamba atakuwa nao na kuwashika mkono siku zote.

Mhe. Samia amewahakikishia nchi marafiki na majirani wa Tanzania kuwa Tanzania itaendelea kuwa jirani mwema na mshirika mzuri katika ushirikaino wa kikanda na kimataifa, na kwamba uhusiano wake utaimarika Zaidi katika kipindi chake cha uongozi.

Katika salamu zao, Marais 9 wa nchi mbalimbali za Afrika wamemshukuru Hayati Dkt. Magufuli kwa utumishi wake wakati wa uhai wake ambapo alioneshas mfano wa namna Afrika inavyoweza kujiamulia mambo yake yenyewe, kujitegemea, kujenga uchumi wake, kupiga vita rushwa na kuwapigania watu wake.

Wamempongeza Mhe. Rais Samia kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wamemhakikishia ushirikiano na uhusiano mzuri katika kipindi chote cha uongozi wake.

Dkt. John Pombe Magufuli alifariki dunia tarehe 17 Machi, 2021 Jijini Dar es Salaam kwa maradhi ya moyo na atazikwa tarehe 26 Machi, 2021 nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.