• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

RAIS SAMIA ANAPENDA KUFANYA KAZI NA VIONGOZI WA DINI - DKT. BITEKO

Imewekwa tarehe: July 1st, 2025

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anapenda kufanya kazi na viongozi wa dini kwa kuwa anawaongoza wananchi wenye dini ambao dini zao wanaziheshimu na hivyo asingependa kuona haki zao zinanyimwa kwa namna yoyote ile.

Dkt. Biteko aliyasema hayo jijini Dodoma wakati akimwakilisha  Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

“Mheshimiwa Rais Samia anapenda kufanya kazi na viongozi wa dini na ninyi ni mashahidi amekuwa akiwaalika ili tuzungumze masuala mbalimbali ya kitaifa ingekuwa ni mtu anayejifungia ndani na akasema analo jeshi, sheria, katiba na vyombo vya ulinzi basi nitafanya kazi nadhani hivi ingekuwa ngumu sana lakini yeye amesema milango yetu iwe wazi tuzungumze na viongozi wa dini kwa ajili ya kutafuta mustakabali wa nchi yetu pale ambapo tunadhani hatuendi sawasawa,” amesema Dkt. Biteko. 

Akijibu hoja za CCT, Dkt. Biteko alisema kuwa imekuwa desturi ya nchi kuwa na waangalizi wa ndani kwenye Uchaguzi Mkuu na kuwa ni imani yake kuwa Tume Huru ya Uchaguzi itawalika waangalizi wa ndani ikiwa ni pamoja na asasi za kiraia. Hata hivyo amesisitiza Tume Huru ya Uchaguzi iachiwe uhuru wake wa kufanya kazi zake. 

Aliwahakikishia kuwa Serikali inatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na taasisi zote za dini ikiwemo makanisa na kusema kuwa tangu Uhuru mwaka 1961, Taasisi za dini zimeendelea kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kuwanufaisha watu wengi kote nchini. 

“Tunawapongeza sana na tunawashukuru sana kwa mchango wenu. Tafiti zinaonesha kuwa Taasisi za dini Barani Afrika huchangia kati ya asilimia30 hadi 70 ya maendeleo ya sekta ya afya. Kidunia, kwa mfano katika elimu, Vyuo kama University of Edinburgh - (Scotland), Oxford University - Uingereza na University of Kwa Zulu - Natal Afrika ya Kusini vilianzishwa na Taasisi za dini,” alisema Dkt. Biteko.

Aliendelea kuzungumzia mchango wa taasisi za dini katika kuzalisha wataalamu wa fani mbalimbali duniani ambao wanaendelea kuiokoa dunia kutoka katika matatizo na majanga mbalimbali akitolea mfano Taasisi ya World Coucil of Churches na World Vision kwa kutoa huduma za kibinadamu duniani kote bila kubagua tofauti zilizopo za dini, rangi, kabila na jinsia.

Katika kutambua mchango wa viongozi wa dini Afrika na duniani kote, Dkt. Biteko alielezea haiba ya Mwanatheolojia Muanglikana kutoka Afrika Kusini, Hayati Baba Askofu Desmund MpiloTutu kama kiongozi wa dini mwenye upendo, mpendahaki na amani, ambaye amechangia kutetea haki za binadamu na kupambana dhidi ya u baguzi na hivyo kusaidia kuleta maendeleo na usawa kwa nchi ya Afrika Kusini na dunia kote.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikistro Tanzania, Baba Askofu, Dkt. Fredrick Shoo alipongeza usikivu wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na juhudi za Serikali za kudumisha demokrasia kwa kuruhusu mikutano ya hadhara sambamba utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.

Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Baba Askofu Dkt. Shoo alisema kuwa CCT inahimiza maadili ya kisiasa na utulivu wa jamii ikiwa ni pamoja na kampeni zisizo za kuvunjiana heshima bali zinazoweka mbele maslahi ya Taifa na kupinga vitendo vyote vya rushwa.

“Uchaguzi ni daraja la amani na maendeleo si chanzo cha mifarakano, jamii idumishe amani, mshikamano na uzalendo wa kila mmoja kwa nafasi yake. Pia Tume Huru ya Uchaguzi iendelee kusimamia haki kwa kushirikiana na waangalizi wa ndani amesema ,” Baba Askofu Shoo.

Alibainisha kuwa CCT itaendelea kushirikiana na Serikali kuleta maendeleo ya jamii hivyo ameiomba Serikali itoe unafuu wa kodi na kutotoza ruzuku kwa misaada inayotolewa na wahisahi ili kuboresha ubora wa huduma na kuwafikia wananchi.

Katibu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji Dkt. Moses Matonya alisema kuwa CCT ni Jumuiya inayounganisha madhehebu wanachama 12 na mashirika ya kikristo 14. Aidha, katika Mkutano huo jumla ya wajumbe waliohudhuria ni 224 kati ya wajumbe wote 280.





Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Serikali yaboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza- Mwambene

    August 18, 2025
  • Afisa elimu mkoa wa Dodoma akagua maandalizi ya Juma la elimu ya watu wazima

    August 17, 2025
  • Wafanyabiashara wa mkoa wa Dodoma watangaziwa fursa za biashara nchini indonesia

    August 16, 2025
  • Wafugaji waaswa kufuga kwa kuzingatia uwezo wa malisho ili kupata tija

    August 15, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.