• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Rais Samia apandisha posho ya safari za ndani na malipo ya kazi maalum kwa watumishi wa umma

Imewekwa tarehe: May 27th, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameendelea ‘kuupiga mwingi’ kwa kutoa kibali cha kurekebisha posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa Watumishi wa Umma na kiwango cha malipo ya kazi maalum (Extra Duty) kwa Watumishi wa Umma nchini ambapo utekelezaji wake unaanza rasmi tarehe 01 Julai, 2022.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro jijini Dodoma wakati wa Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma chenye lengo la kutathmini utendaji kazi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Dkt. Ndumbaro amesema kutokana na kibali hicho cha Mhe. Rais, posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa Watumishi wa Umma kwa kiwango cha juu imepanda kutoka shilingi 120,000/= hadi 250,000/= na kiwango cha chini kutoka shilingi 80,000 hadi 100,000/=.

Ameongeza kuwa, kiwango cha malipo ya kazi maalum (Extra Duty) kwa Watumishi wa Umma kimeongezeka kwa ngazi zote, ambapo kwa ngazi ya chini kimepanda kutoka shilingi 15,000/= hadi 30,000/=, kwa ngazi ya kati kimeongezeka kutoka shilingi 20,000/= hadi 40,000/= na kwa ngazi ya juu kimeongezeka kutoka shilingi 30,000 hadi 60,000/=.

Dkt. Ndumbaro amesisitiza kuwa, viwango hivyo vipya vitalipwa na Serikali kupitia bajeti iliyoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023, hivyo taasisi zisiombe nyongeza ya bajeti ili kuwalipa viwango hivyo watumishi wake.

Kufuatia ongezeko hilo, Dkt. Ndumbaro ametoa wito kwa Watumishi wa Umma wote nchini kufanya kazi kwa bidii, maarifa, weledi na nidhamu ya hali ya juu ili kuunga mkono kwa vitendo jitihada za Mhe. Rais za kuboresha masilahi wa Watumishi wa Umma.

“Watumishi wa Umma tuwajibike kwa hiari bila kushurutishwa, tuwe wabunifu zaidi ili kutoa mchango katika maendeleo ya taifa na ustawi wa nchi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuhakikisha tunatatua kero zinazowakabili wananchi,” Dkt. Ndumbaro amesisitiza.

Sanjari na hilo, Dkt. Ndumbaro ametoa wito kwa Wakuu wa Utumishi wa Umma hususani walio katika halmashauri na taasisi zenye matawi kuwatembelea watumishi wanaowasimamia kwenye maeneo yao ya kazi ili waweze kubaini changamoto zinazowakabili na kuzitatua ili kuondoa changamoto ya watumishi kusafiri umbali mrefu kwenda makao makuu kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi changamoto zao.

“Mkiwafuata katika vituo vyao vya kazi mtawasaidia kuwapunguzia gharama za kusafiri kwenda makao makuu ya wilaya, mkoa au makao makuu ya nchi kwa ajili ya kutatua changamoto zao kwani nyie viongozi mkiwatembelea Serikali ndio itawagharamia,” Dkt. Ndumbaro amefafanua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani amekuwa mstari wa mbele kuboresha stahiki za Watumishi wa Umma nchini ili kuwajengea ari na morali ya kutoa huduma bora kwa wananchi na hatimaye wananchi wajivunie uwepo wa Serikali yao.

Chanzo: fullshangweblog

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.