RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwa njia ya mtandao mkutano wa Wakuu wa Nchi na Mashirika ya Kimataifa uliojadili namna ya kuokoa uchumi wa nchi za Afrika kufuatia madhara yaliyosababishwa na janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19) na kufanyikakwa Jijini Paris kwa wito wa Rais wa Ufaransa Mhe. Emmanuel Macron.
Mkutano huo umehudhuriwa na Marais wa nchi za Angola, Burkina Faso, DRC, Code d'Ivoire, Misri, Ethiopia, Ghana, Mali, Mauritania, Msumbiji, Nigeria, Rwanda, Senegal, Sudan, Togo, Tunisia, Italia, Hispania na Umoja wa Ulaya wakati Tanzania, Kenya, Afrika Kusini, Uholanzi, Ujerumani, China na Japan zimwshiriki kwa njia ya mtandao.
Mashirika ya Kimataifa yaliyoshiriki ni Umoja wa Mataifa (UN), Shirika la Fedha Duniani (IMF), Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo Duniani (OECD), Shirika la Biashara Duniani (WTO), Benki ya Dunia na mabenki mbalimbali.
Mhe. Rais Samia ameungana na Marais wengine Duniani kumpongeza Mhe. Rais Macron kwa kuitisha mkutano huo ambao wamesema umelenga sio tu kusaidia uchumi wa Bara la Afrika bali kuokoa maisha ya binadamu waliopo Afrika kutokana na kuathirika na madhara yaliyosababishwa na Korona.
Vile vile Mhe. Rais Samia amesema Tanzania kama ilivyo kwa nchi zingine duniani imekumbwa na madhara ya ugonjwa wa Korona ambayo yameathiri biashara, utoaji wa huduma za kijamii, kushuka kwa mapato, kupoteza maisha na kupoteza ajira mambo ambayo yamewaadhiri zaidi wanawake, vijana na watoto.
Aidha, amebainisha kuwa kutokana na athri hizo, Tanzania ambayo hivi karibuni imeingia katika uchumi wa kipato cha kati imechukua hatua mbalimbali ili kulinda uchumi wake na hasa miradi mikubwa ya kimkakati inayoitekeleza zikiwemo kuimarisha zaidi mazingira ya kufanya biashara ili kuvutia uwekezaji zaidi nchini.
Mhe. Rais Samia ametoa wito kwa washiriki wa mkutano huo hususani Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua stahiki kuokoa uchumi wa nchi za Afrika zikiwemo mashirika ya fedha ya kimataifa kuongeza mikopo yenye masharti nafuu kwa miradi ya maendeleo ya nchi za Afrika na kusaidia sekta binafsi katika Bara la Afrika kwa kuiwezesha kupata mikopo nafuu ili kukuza biashara hasa ndogo na za kati ambazo ndio nguzo muhimu ya uchumi.
Hatua nyingine ni kusamehe mikopo ama kuongeza muda wa ulipaji wa mikopo ambayo nchi za Afrika zinadaiwa na kuchangia fedha katika bajeti za nchi za Afrika kutokana na nchi hizo kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapatoya ndani.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.