RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza Wakuu wa Mikoa kuhakikisha fedha zilizopangwa kutekeleza mipango ya lishe zinatolewa kwa wakati.
Rais Samia ametoa agizo hilo leo tarehe 30 Septemba, 2022 wakati akihutubia Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Sita ya Mkataba wa Lishe uliofanyika ukumbi mpya wa kisasa wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliopo mji wa Serikali Mtumba.
Aidha, Rais Samia amesema kuwa kuweka mpango lishe mikoani hautekelezwi ipasavyo hivyo Wakuu wa Mikoa wanapaswa kujipanga na kuongeza jitihada za kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za lishe bora na kuzipa kipaumbele ili zilete tija.
Rais Samia ameelekeza sekta zinazoguswa na utapiamlo ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, afya na biashara kuweka mikakati ya kuhakikisha vyakula vinavyohitajika katika kukamilisha lishe vinapatikana na kuviongezea virutubisho hasa katika ngazi za chini.
Hali kadhalika, Rais Samia ameiagiza Wizara ya Afya kuifanyia mabadiliko Sera ya Taifa ya Lishe ya mwaka 1992 ambayo imepitwa na wakati ili iendane na hali halisi ya mipango ya sasa hivi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.