RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Watunza kumbukumbu na Nyaraka za umma kuzingatia weledi wa kazi yao kwa kuhakikisha wanatunza Siri za Serikali kwa maslahi ya Taifa.
Rais Samia amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 10 wa Chama Cha Taaluma na Menejimenti ya utunzaji Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania uliofanyika ukumbi wa AICC Mkoani Arusha.
Aidha Rais Samia ameonyesha kutofurahishwa na kuvuja kwa taarifa nyeti za Serikali kwenye mitandao ya kijamii ambapo amewaelekeza wanataaluma kuangalia kwa jicho la tatu suala Hilo.
Kuhusu suala la matukio ya kupotea kwa Nyaraka na taarifa, Rais Samia ametoa wito kwa watunza Kumbukumbu hao kuongeza umakini katika usimamizi na uhifadhi thabiti wa Nyaraka hizo kwakuwa kosa moja linaloweza kufanywa na mtunza Kumbukumbu linaweza kugharimu Maisha ya wengi.
Pamoja na hayo Rais Samia amesema Serikali itaendelea kuboresha maslahi ya watunza Kumbukumbu ikiwa ni pamoja na kupanda kwa Madaraja.
Kutokana na unyeti wa kazi ya utunzaji Kumbukumbu, Rais Samia ameelekeza mkutano wa mwakani uende sambamba na ulaji kiapo kwa watunza Kumbukumbu na makatibu muhtasi.
Hata hivyo Rais Samia amewapatia eneo Chama Cha Watunza Kumbukumbu na Nyaraka kwaajili ya Ujenzi wa Kituo Cha Maarifa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.