RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo Disemba 4, 2021, ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Pili katika barabara za Kilwa, Chang'ombe, Sokoine na Kawawa jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo imefanyika katika Karakana Kuu ya Mradi huo, Mbagala Rangitatu jijini Dar es Salaam.
Mradi huo unasimamiwa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) na unatekelezwa kwa fedha za Mkopo wa Masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wa sh. bilioni 327.351 na fedha za serikali sh. bilioni 40.679.
Muonekano wa Barabara ya Kilwa, Kituo pamoja na Karakana ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika eneo la Mbagala barabara ya Kilw mkoani Dar es Salaam.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.