RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Sheria inayotarajia kufika tamati Februari Mosi mwaka 2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri alitoa taarifa hiyo mbele ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma lililokutana Januari 26, mwaka huu kwa ajili ya kupokea taarifa ya maendeleo kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/2022.
Mkuu huyo wa Wilaya aliwaeleza wajumbe wa baraza hilo na wananchi kwa ujumla kuwa, hafla ya kufunga wiki ya sharia itafanyika katika viwanja vya Chinangali na kutoa wito kwa madiwani na wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika tukio hilo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.