RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, siku ya Jumanne ya Juni 8, 2021 anatarajiwa kukutana na kuzungumza na Wanawake wa Mkoa wa Dodoma kwa niaba ya wakina mama wa nchi nzima katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Anthony Mtaka alipowaita na kuongea na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dodoma.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa wanatarajia zaidi ya wanawake elfu kumi watahudhuria mkutano huo wakiwemo Wabunge wanawake wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kujali itikadi zao, pia waheshimiwa madiwani walioko kwenye mkoa wa Dodoma, watumishi wanawake wa kada mbalimbali, wamama wajasilimali, mamantilie, wamama wakulima na wafugaji na kila aina ya uwakilishi wa akina mama.
Aidha, Mhe. Mtaka ametoa wito kwa Wanawake wa Mkoa wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kushiriki kikao hicho ili kupata fursa ya kumsikiliza Mhe. Samia. Vile vile, amewataka Wanawake waliopo mikoa mingine ya Tanzania kufuatilia Mkutano huo wa Mhe. Rais Samia na Wanawake wa Mkoa wa Dodoma kupitia vyombo vya Habari vikiwemo vituo vya luninga, magazeti, redio na mitandao ya kijamii.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.