"Kwa masikitiko makubwa natangaza kifo cha kiongozi mkubwa Afrika, Daniel Toroitich arap Moi, rais wa pili wa Kenya. Raisi mstaafu amefariki katika Hospitali ya Nairobi mapema asubuhi ya leo Februari 4 akiwa na familia yake" amethibitisha Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Naye msemaji wa Mzee Moi Lee Njiru ameongeza kuwa, "...alikuwa Nairobi Hospital ambapo alilazwa tarehe 10 mwezi wa kumi mwaka uliopita, hiyo ni zaidi ya miezi mitatu,".
Kwa mujibu wa Njiru mipango yote ya mazishi ipo chini ya jeshi la Kenya kwa kuwa Mzee Moi alikuwa amiri jeshi mstaafu wa nchi hiyo.
Mzee Moi alizaliwa Septemba 2, 1924 na alitawala Kenya kwa miaka 24 kutoka 1978 mpaka 2002.
Tangazo kutoka Ikulu limesema kuwa mzee Moi, hata baada ya kuondoka madarakani aliendelea kulitumikia taifa la Kenya na Afrika kwa kuwafundisha viongozi wa Kenya na nje ya Kenya, akiendelea kushiriki kwenye maendeleo ya miradi mbalimbali na kazi za misaada akiihubiri amani, upendo na umoja barani Afrika na duniani.
Mzee Moi aliiongoza Kenya kuelekea kurudisha mfumo wa vyama vingi na katika vipindi vingine vingi vya changamoto; na kumalizika kwa mchakato wa kukabidhi madaraka kwa amani mwezi Desemba mwaka 2002, wakati huo mchakato ambao ulikuwa nadra kufanyika Afrika, ambao uliweka mfano barani Afrika na nje ya bara tangu wakati huo.
''Haiba yake inaishi Kenya hata leo. Filosofia ya Nyayo kuhusu 'amani, upendo na umoja' ilikuwa wimbo wake kipindi chake kama kiongozi wa nchi na serikali''. Ilieleza taarifa ya Ikulu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.