• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

RC Mtaka ataka maafisa ardhi kuacha dhuluma

Imewekwa tarehe: July 7th, 2022

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amewataka baadhi ya Maafisa Ardhi kuacha dhuluma na badala yake wamrudie Mungu kwa kwenda kuwahudumia wananchi kwa haki bila upendeleo

Pia amewataka Maofisa wa idara hiyo waliohamishiwa Jijini Humo kwenda kutatua migogoro ya Ardhi kwa Wananchi na kwamba hicho ndicho kitakuwa kipimo cha utendaji wao wa kazi.

Mtaka ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma, ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akizungumza na watendaji wapya na wale wa zamani wa idara ya Ardhi kwenye kikao cha kuwajengea uwezo Jijini Dodoma.

”Baadhi ya wataalamu wa Idara ya Ardhi Jijini Dodoma wametengeneza migogoro mingi kwa wananchi kwa kutoa hati ya kiwanja kimoja kwa watu zaidi ya wawili, huku wakiwapangia nini cha kufanya kwenye maeneo yao.

Unakuta mtu ana shamba lake wapimaji wanakwenda kupima kisha wanamuondoa pale wanamwambia hapa kapewa mtu mwingine na mhusika atatafutiwa sehemu nyingine, nyie nyie hebu muogopeni Mungu vilio vya wananchi hawa ukivisikiliza vinakuumiza sana, fikiri kama shamba hilo lingekuwa la baba au babu yako ungemfanyia vitendo kama hivyo au ndiyo mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mchungu?” Ameuliza Mtaka.

Kwa Upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amesema kuwa mara nyingi amepokea malalamiko toka kwa wananchi kuwa wamejibiwa kuwa mafaili hayaonekani na anapomuita mhusika anabaki akiwafokea.

“Tuambieni ukweli tu mtu anapojibiwa kuwa faili lake halionekani maana yake kiwanja hicho kipo sokoni kinatafutiwa mtu mwingine auziwe na ndiyo sababu ya kiwanja kimoja kumilikiwa na watu zaidi ya mmoja”, amesema.

“Mara nyingi nilipoletewa kesi ya namna hiyo nikimwita mhusika akijiumauma kwenye majibu huwa namwambia aniandikie kimaandishi kuwa faili la fulani halionekani, atakwambia ngoja nikajaribu tena baadae anakuja nalo na kusingizia kuwa lilichanganywa kwenye ofisi nyingine”. Amesema Mwamfupe.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri amesema ili kukomesha migogoro hiyo na kuondoa ubabaishaji katika uuzaji wa viwanja jiji hilo liweke kwenye mfumo wa kidigitali kila kitu kinachoihusu idara ya ardhi pamoja na orodha ya wamiliki na waombaji wapya.

Awali Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru, alisema makampuni ya upimaji yalichangia migogoro hiyo na kulitia jiji hasara kutokana na kupima viwanja vidogo kwa lengo la kupata viwanja vingi ili waweze kulipwa zaidi.

“…mfano unakuta eneo ni la kupima ukubwa wa mita za mraba 2000 au zaidi wao wanapima ukubwa wa mita za mraba 600 au 800, ili walipwe fedha za viwanja vingi lakini bila ufanisi, hivyo tangu sasa hatutatumia makampuni ya upimaji”, amesisitiza Mafuru.

“Tumenunua vifaa vya kupimia vya zaidi ya shilingi milioni 40 na magari matatu kwa ajili ya shughuli za kupimia viwanja”. Alisema Mafuru.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza katika kikao cha kuwajengea uwezo  watendaji wapya na wale wazamani wa idara ya Ardhi kilichofanyika Jijini Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri ,akizungumza kwenye  kikao cha kuwajengea uwezo  watendaji wapya na wale wazamani wa idara ya Ardhi kilichofanyika Jijini Dodoma.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Prof.Davis Mwamfupe,akizungumza kwenye  kikao cha kuwajengea uwezo  watendaji wapya na wale wazamani wa idara ya Ardhi kilichofanyika Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru, akielezea mikakati ya jiji hilo kumaliza migogoro ya ardhi wakati wa  kikao cha kuwajengea uwezo watendaji wapya na wale wa zamani wa idara ya Ardhi kilichofanyika Jijini Dodoma.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.