Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) ameelekeza ufundishaji wa somo la Michezouimarishwe kuanzia shule ya awali, msingi, sekondari na vyuo ili kujenga haliya kujiamini na kuwa mahiri kimwili na kiakili.
Mhe. Majaliwa ameyasema hayo leo wakatiakifungua mashindano ya michezo na taaluma yajulikanayo kama UMISSETA naUMITASHUMTA yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.
Ameeleza michezo ni muhimu zaidi kwa makuzina maendeleo ya taaluma ya watoto na vijana na ina mchango mkubwa katikakuimarisha afya ya mwili na akili.
“Watafiti wamethibitisha kuwa michezo kwamadarasa ya awali kwa maana ya miaka 3 – 6 ni muhimu zaidi katika kuongezauwezo wa mzunguko wa damu katika ubongo (kuongezeka kwa mishipa ya damu) namaendeleo ya afya na makuzi ya watoto kwa ujumla wake hivyo ni vyema tukajikitakumjenga mtoto huyu kuanzia kwenye ngazi ya awali;
Bila shaka sote tunaelewa kuwa binadamuhawezi kuwa na akili bora kwenye mwili dhaifu na afya bora inaweza kujengwavizuri zaidi kwa kushiriki katika michezo hivyo tujikite katika kutengenezavizazi vitakavyokua mahiri kwenye michezo wakati wote maisha yao.” Amesema Mhe.Majaliwa kwa msisitizo.
Majaliwa alibainisha kuwa katika siku za hivikaribuni kumekuwepo na mafanikio makubwa ya vijana waliyoyapata kupitia michezona wengi ni wa hapa hapa Tanzania, kama vile Mbwana Samata.
“Kwa hawa wachache wanatuonyesha picha kubwaya namna ambavyo vijana wetu wengi wanaweza kufanikiwa kupitia michezo na sanaatuongeze nguvu katika eneo hili,” amesema Majaliwa.
Aidha amesema Michezo na Sanaa vikiwekewamipango sahihi vina nafasi kubwa ya kuchangia na kujenga uchumi endelevu waTaifa na watu wake.
“Sekta hizi ni fursa kubwa kwa vijana wetukujiajiri, kuajirika na kuutambulisha utamaduni wetu ndani na nje ya mipaka yanchi yetu,” amefafanua zaidi Waziri Mkuu.
Hivyo basi, amewataka wanafunzi wotewanaoshiriki katika mashindano hayo kutoridhika na hatua waliyofikia kwenyemashindano hayo bali yawe mwanzo wa kujiimarisha katika michezo na sanaa ilikulitangaza Taifa kupitia michezo na sanaa.
Vile vile, amewakumbusha washiriki wa mashindanihayo amesema “Matarajio ya wengi ni kuona mkionyesha uwezo wenu kwa nidhamu yahali ya juu na kuiletea mafanikio mikoa yenu na taifa kwa jumla,”
Waziri Mkuu pia amezitaka Wizara zinazohusikakurudisha mafunzo ya michezo katika vyuo vya Butimba na Mtwara ili kufundishawalimu watakaoweza kuwapa wanafunzi mafunzo sahihi ya michezo.
Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa, amesema wanakusudia kuanzisha Vituovya kulea vipaji katika shule mbalimbali ili kuhakikisha kuwa vipaji vya watotovinaendelezwa kuanzia umri mdogo.
Naye, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe.Davidi Silinde ameelezea malengo ya mashindano hayo kuwa ni kujenga umoja wakitaifa, mshikamano na upendo baina ya wanafunzi wangali katika umri mdogo, kuimarishataaluma ya michezo kwa wanafunzi ili kuwajengea ujuzi na maarifa na kuwa mahiriwanapoendelea kukua pamoja na kujenga umoja, uzalendo na mshikamano miongonimwa wanafunzi, walimu na wadau wa michezo nchini.
Pia ameongeza kuwa mashindano hayoyatawajengea watoto ukakamavu na umahiri katika michezo pamoja na kuibua nakuendeleza vipaji vya wanafunzi wangali bado wachanga na kujenga dhana yauvumilivu na ustahimilivu.
Mashindano hayo yamebeba kauli mbiu ya “Michezo,Sanaa na Taaluma kwa maendeleo ya viwanda” na jumla ya wanamichezo 3,600 kutokamikoa 26 wanashiriki kwenye michezo ya UMITASHUMTA na wanamichezo 3,800 kutokakatika mikoa 28 ya Tanzania Bara na Visiwani wanashiriki katika michezo yaUMISSETA, mashindano hayo yatafungwa Julai 4, 2021.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.