MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule ametuma salamu za Mkoa kwa wanafunzi wote wa Darasa la Saba wa mkoani Dodoma wanaotarajiwa kufanya mtihani wao wa taifa wa kuhitimu elimu ya msingi hapo kesho tarehe 5/10/2022.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amewatakia mtihani mwema wanafunzi hao huku akiahidi kuhakikisha mitihani hiyo inafanyika kwa utulivu na amani katika mkoa wa Dodoma kwani anaamini moja ya mambo yanayoweza kusaidia mwanafunzi kufanya vyema ni pamoja na hali ya amani na utulivu kitu ambacho mkoa wamejipanga kusimamia vyema zoezi hilo.
“…niwasisitize na kuwapa moyo wanafunzi jwote wa mkoa wa Dodoma kuwa kila mmoja ahakikishe anafanya mtihani wake kwa utulivu na amani kwani tunaaamini Dodoma ina wanafunzi bora wengi na tunatarajia mtamaliza mitihani yenu salama na kufaulu vizuri” alimalizia RC Senyamule katika salamu zake.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.