• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Ruzuku ya Mil. 250 yatolewa kwa wabunifu wa matumizi ya bora ya Nishati

Imewekwa tarehe: September 17th, 2025

Serikali kupitia Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP), imetoa ruzuku ya jumla ya shilingi milioni 250 kwa wabunifu kumi waliofanya vizuri katika Mashindano ya Ubunifu na Ufanisi wa Matumizi Bora ya Nishati. 

Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga amekabidhi ruzuku hiyo akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mha. Felchesmi Mramba katika hafla iliyofanyika Septemba 12, 2025 jijini Dar es Salaam. 

Hafla hiyo iliwakutanisha wabunifu mbalimbali waliobobea katika nyanja ya ufanisi wa matumizi bora ya nishati katika maeneo matatu ambayo ni ubunifu kwenye vifaa vinavyotumia umeme kidogo, ubunifu kwenye miundombinu ya majengo yanayotumia umeme kidogo pamoja na ubunifu wa vifaa vinayoonesha matumizi ya umeme.

Mha. Luoga alifafanua kuwa wabunifu waliojitokeza kushindanishwa walikuwa wengi lakini baada ya uchambuzi wa kina kufanyika jumla ya washindi 10 walipatikana. 

Mha. Luoga alitanabaisha kuwa katika jitihada za kuhamasisha matumizi bora ya nishati nchini, serikali ilishazindua mikakati mbalimbali ya kitaifa ikiwemo Mkakati wa Taifa wa Matumizi Bora ya Nishati pamoja na Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano kuhusu Nishati Safi ya Kupikia.

Alisema lengo kuu la mikakati hiyo ni kuchochea matokeo chanya ya matumizi bora ya nishati kwa kuzingatia ubunifu unaofanywa na vijana katika kuendeleza teknolojia zinazochangia ustawi wa sekta ya nishati nchini.

Aidha, Luoga alibainisha kuwa kuongezeka kwa ubunifu wa vifaa vinavyotokana na matumizi bora ya nishati kutachangia mafanikio makubwa kwa taifa hasa katika kuimarisha upatikanaji wa nishati endelevu na rafiki kwa mazingira.

“Serikali itaendelea kuwafuatilia na kuwaunga mkono vijana wabunifu katika teknolojia ya matumizi bora ya nishati kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, ikiwemo Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)” alisema Mha. Luoga.

Katika hatua nyingine, alibainisha kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati, imeishauri UNDP kusaidia katika kuweka mifumo ya matumizi bora ya nishati katika majengo ya Serikali yaliyo Mji wa Serikali wa Mtumba.

Hatua hiyo inalenga kuonesha mfano wa matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira katika taasisi za umma, sambamba na kuhamasisha matumizi bora ya nishati kwa ufanisi katika maeneo mengine ya serikali.

Kwa upande wake, Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), John Rutere alisisitiza umuhimu wa ubunifu wa ndani katika kuharakisha maendeleo ya jamii na kuimarisha mabadiliko ya nishati nchini Tanzania.

“Ninawapongeza wabunifu wa kike waliokuwa miongoni mwa washiriki wa mashindano ya ubunifu wa matumizi bora ya nishati kwani ushiriki wao unaonyesha ongezeko la ushirikishwaji wa wanawake katika sekta ya nishati na maendeleo ya taifa kwa ujumla” alisema Rutere.

Alieleza kuwa hatua ya kuwawezesha na kuinua wabunifu, hususan wanawake, itaendelea kupewa kipaumbele ili kuhakikisha teknolojia bunifu za matumizi bora ya nishati zinaibuliwa kwa kasi katika mataifa mbalimbali ya Afrika.

 


  



Matangazo

  • TANGAZO LA MABADILIKO YA TAREHE YA USAHILI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA WASIMAMIZI JIMBO LA MTUMBA October 03, 2025
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA- DODOMA MJINI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA MAKARANI WAOGOZAJI WAPIGA KURA October 03, 2025
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Rc Senyamule awasihi wawekezaji sekta binafsi kuwekeza Dodoma

    October 03, 2025
  • CCTV kamera mwarobaini wa wavunjifu wa sheria jiji la Dodoma

    October 02, 2025
  • Wadau wa afya wapongezwa kwa juhudi zakudhibiti vifo vya wajawazito

    October 01, 2025
  • UONGOZI WA KLABU YA MICHEZO OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAKUTANA NA RAS KAZUNGU

    September 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.