WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa alisema kuwa Sekta ya elimu ni wakala wa mabadiliko katika jamii kiuchumi, kiteknolojia na kiutamaduni katika kuleta maendeleo ya nchi.
Amesema hayo wakati wa mkutano wa wadau wa Sekta ya Elimu mkoani Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Biblia-TAG jijini Dodoma.
Amesema kuwa utoaji wa elimu bora kwa Watanzania ni moja ya vipaumbele vya nchi katika kuleta maendeleo. “Ili kufanikisha haya tunahitaji sekta hii kuwa bora, imara, inayokidhi mahitaji ya jamii kwa kuwapa vijana maarifa na ujuzi wa kukabiliana na matatizo ya kijamii, kitaifa na kimataifa”.
Majaliwa alisema kuwa Rais Dkt. Suluhu Samia ni mdau namba moja wa sekta ya elimu na ndio maana katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake amewekeza katika kuweka mazingira bora ya utoaji elimu na kuhakikisha Serikali inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo katika Sekta ya Elimu.
“Ninaamini sisi sote ni mashuhuda wa jinsi Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan, katika kipindi cha uongozi wake alivyotekeleza kwa vitendo azma ya kuhakikisha elimu bora inapatikana kwa Watoto wote wa Kitanzania bila kujali jinsia wala hali ya kiuchumi”.
Aidha aliongezea kwa kusema kuwa baadhi ya maeneo ambayo Rais Dkt. Samia ameyasimamia kikamilifu ni Mpango wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu, Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi, Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu, Mapitio ya Sera Ya Elimu na Mafunzo.
Maeneo Mengine ni Kuimarisha Usimamizi wa Sekta ya Elimu kwa kutoa vyombo vya usafiri kwa viongozi wasimamizi wa elimu pamoja na wathibiti ubora wa shule, Kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji Elimu na kutoa Mafunzo kwa walimu kazini (MEWAKA) kwa ajili ya kuwajengea uwezo na umahiri katika kutimiza majukumu yao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.